Publisher Food and Agriculture Organization of the United Nations
Ugonjwa unapotokea, na dawa aina ya antibayotiki zikashindwa kufanya kazi, unaweza kupoteza Mifugo yako yote kutokana na ugonjwa. Hii pia inahatarisha afya yako na familia yako kwani ugonjwa unaweza kusambaa kati ya Mifugo na binadamu.
Okoa maisha kwa kufuata ushauri uliopohapa chini kuanzia leo!
Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha dawa zishindwe kutibu magonjwa;
• Kutumia dawa isiyo sahihi wakati wa matibabu husika au matumizi holela ya
dawa.
• Vimelea vinavyosababisha maambukizi vinakuwa sugu dhidi ya dawa- kitendo
hiki huitwa “Usugu wa Dawa”.
Kila tunapotumia dawa mfano Antibayotiki kutibu maambukizi kwa binadamu,
mifugo na mimea, vimelea hawa hupata fursa ya kubuni mbinu mbalimbali za
kukabiliana na tiba na kusabababisha dawa zipungue uwezo wa kutibu kadri muda
unavyoenda.
Usugu wa dawa ni moja ya sababu kubwa inayosababisha dawa nyingi muhimu
kushindwa kutibu ipasavyo. Tusipokuwa na dawa zinazofanya kazi vema, watu
wengi, mifugo na mimea itakuwa katika hatari kubwa ya kufa kutokana na
maambukizi.
Lakini tunaweza kuchukua hatua sasa ili kuziwezesha dawa hizi kuendelea
kufanya kazi ipasavyo.
...