View this book in English Storytelling
Sign up for news and free books by email!
Usimulizi wa Hadithi
Chombo cha Kuendeleza amani na Usomi
Written by
Publisher Feed the Minds
Published 2011
sw
Pages 36
Download
0.7 MB
Usimulizi wa hadithi una nafasi muhimu katika jamii ya Afrika, hasa katika familia. Kitamaduni, watoto kujifunza kuhusu mila, dini na utamaduni wanaposikiliza hadithi kutoka kwa wazazi wao. Hadithi huwasaidia watu kuelewa dunia na watu wengine. Hata hivyo, baadhi ya hadithi kuhamasisha ukabila, na hadithi zinaweza kutumika kutekeleza dhuluma na mashinikizo. Hivyo basi, uteuzi makini ni muhimu. Hadithi miongoni mwa watu wazima mara nyingi hutumika kwa kuburudisha, bali pia zinaweza kuwa chombo cha nguvu cha kujenga amani katika familia na jamii zilizogawanyika. Hadithi hutoa fursa ya kutatua migogoro na kusaidia watu kusamehe na kupatanishwa. Usimulizi wa hadithi unaweza kuwa wa thamani katika kuwafariji wanao omboleza msiba au hasara zozote. Msimulizi wa hadithi anaweza kunufaika kwa kuhisi kuwa hayuko ‘peke yake’ na ya kwamba kuna watu ‘waliosikiliza’ masaibu yake. Anayesimuliwa anaweza kusikia na kuelewa matukio kupitia kwa macho na masikio ya mtu mwingine. Hatua za usumulizi wa hadithi zikiwezeshwa kiustadi, zinaweza kusaidia jamii kuandaa mipango ya uponyaji na maendeleo. Sanaa ya usimulizi wa hadithi imekuwa ikipotea katika baadhi ya jamii kwa njia ya vita na migogoro, kutokana na kuvunjika kwa familia au kuongeza kwa teknolojia....
...
Mwakaribishwa kutengeneza nakala za kijitabu hiki na kukitumia katika warsha. Hata hivyo, tafadhali, tambulisha Feed the Minds kila wakati unapokitumia. Pia tunakaribisha maoni kuhusu ya kijitabu hiki na jinsi kilivyotumikiwa. Tafadhali tuma maoni yako kwa info@ feedtheminds.org Nakala zingine za kijitabu hiki zinapatikana kutoka kwa SEM pia PHARP, na pia kwa kusafura tuvuti ya Feed the Minds www.feedtheminds.org
...
Thank you to Feed the Minds
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.