Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Kiswahili 6 Sanifu kwa Shule za Sekondari, Kitabu cha Mwanafunzi, Kidato cha Sita
Kimeandikwa na
Mchapishaji Tan Prints
sw
Kurasa 136
Pakua
Vitabu ambavyo vilitangulia vilikuwa na lengo la kumsaidia mwanafunzi aweze kuzungumza Kiswahili sanifu na kukiandika kwa urahisi. Kwa hiyo, kitabu hiki kinakuja kuviunga mkono vitabu hivyo ili lugha ya Kiswahili iendelee kupiga hatua. Kitabu hiki kitatumiwa katika kidato cha sita mkondo wa lugha ambapo lugha ya Kiswahili ni mojawapo wa masomo makuu. Madhumuni makubwa ya kitabu hiki ni kuwaongoza wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkondo wa lugha kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili na kuimarisha lugha hii. Kitabu hiki kinaundwa na sura nne ambazo ni: FASIHI, MYAMBULIKO WA VITENZI, UAMBISHAJI WA VITENZI NA MANENO YA KISWAHILI, UTUNGAJI (Risala na hotuba). Mwishoni mwa kila sura kumeandaliwa mazoezi ambayo yatawasaidia wanafunzi kufungua akili na kujaribu kuzama katika mada zilizojadiliwa kitabuni. Katika kitabu hiki mkazo ni kueleza maana ya mnyambuliko na uambishaji wa vitenzi kama sehemu moja ya sarufi ambayo haikujadiliwa zaidi katika vitabu vilivyotangulia. Somo hili litamwongezea mwanafunzi ustadi wa lugha hii ya Kiswahili.
...
Shukrani kwa Tan Prints
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.