Mwongozo wa mwalimu kidato cha nne ni kitabu cha kumsaidia mwalimu kufundishia kitabu cha mwanafunzi cha kidato cha nne. Mwalimu ana hiari kufuata na kukubali mpango uliopangwa na waanndishi au kubadilisha sehemu nyingine kwa kufuatana
na ujuzi wa lugha hii, yaani Kiswahili.
Mwalimu anashauriwa ajaribu awezavyo kusoma sehemu ya matayarisho kabla ya kufunza somo lolote. Kutofanya hivyo kutamfanya mwalimu kushindwa kulisomesha somo lake kwa namna na hali ipasayo. Katayarisho hayawezi kabisa kufanywa siku hiyo wala si rahisi kwa vifaa vyote kupatikana siku hiyo hiyo. Kutokana na hayo yote wanafunzi wataweza kusikiliza, kutamka, kuona, kutenda, kusoma na kuandika Kiswahili vizuri zaidi na kwa urahisi kwa sababu mwalimu amejitayarisha vyema.
Kitabu hiki pia, kimetayarishwa kwa ajili ya kurahisisha kazi ya mwalimu ya kufundisha Kiswahili. Tunakuonyesha shabaha za jumla za kila funzo, yanayohitajika kufundishwa kila juma na kila mhula. Namna mwanafunzi na mwanalimu mnavyosaidiana ili somo lenyewe liweze kufikia lengo lake pamoja na vifaa utakavyovitumia kwa kuendeleza somo.
...