Kiwango Kikuu cha Kibinadamu kuhusu Ubora na Uwajibikaji

Faster download

Published Year: 2014

Book Thumbnail

Language: sw

Details: Kitabu hiki kinahusiana na darasa hili: https://kayaconnect.org/course/info.php?id=549 Soma bure mtandoani kwa kiswahili. © Haki zote zimehifadhiwa. Hakimiliki ya maudhui yaliyomo hapa ni ya CHS Alliance, Groupe URD na Mradi wa Sphere. Maudhui haya yanaweza kuchapishwa upya kwa madhumuni ya kielimu, ikiwa ni pamoja na mafundisho, utafiti na shughuli za miradi, maadamu Kiwango Kikuu cha Kibinadamu kinachohusu Ubora na Uwajibikaji kimefuatwa. Ili kutafsiri au kuomba sehemu ndogo au maudhui yote ya Kiwango Kikuu cha Kibinadamu kinachohusu Ubora na Uwajibikaji, ni sharti mhusika apewe ruhusa kwa kutuma barua pepe kwa info@corehumanitarianstandard.org.

Summary: Kila kukicha kote duniani, idadi kubwa ya watu kutoka matabaka mbali mbali huchukua hatua muhimu za kibinadamu - hamu ya kuzuia na kupunguza mateso kwa binadamu janga zinapotokea. Kiwango Kikuu cha Kibinadamu kinachohusu Ubora na Uwajibikaji (CHS) kimeweka Maazimio Tisa ambayo mashirika na watu binafsi wanaohusika katika usaidizi wa kibinadamu wanaweza kutumia kuboresha na kunufaisha usaidizi wanaotoa. CHS pia huwezesha uwajibikaji zaidi kwa jamii na watu walioathiriwa na mikasa: kufahamu maazimio ya mashirika kutawasaidia kuyashinikiza yawajibike. CHS huzipa kipaumbele jamii na watu walioathiriwa na mikasa katika usaidizi wa kibinadamu na kuhimiza kuheshimu haki zao za kibinadamu.