You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Jinsi ya Kuanzisha Maktaba Ndogo ya Jumuiya
Kuelekea Kuleta Mwamko Mpya wa Kujisomea Tanzania
Published 2014
sw
Pages 15
Download
0.9 MB
Mataifa yote ambayo yameweza kupiga hatua za haraka za maendeleo ni mataifa ambayo yameweka mkazo mno katika elimu; katika kusoma; katika kupata maarifa. Tangu enzi za Wagiriki wa kale hadi leo hii jamii ambazo zimeweza kujibadilishia kwa haraka na kwa ubora maisha yao ni jamii ambazo kati yake kulikuwepo na kuthamini vitabu. Hii ni kweli kuanzia Uchina, Ulaya, Marekani, India na hata Afrika. Hata mabadiliko makubwa yaliyosababishwa na ujio wa Mapinduzi ya Viwanda yanaweza kuhusishwa moja kwa moja na upatikanaji wa vitabu kwa urahisi zaidi na kwa watu wengi zaidi. Upatikanaji wa vitabu katika jamii mbalimbali ulisababisha uharaka na urahisi wa kupatikana maarifa kutoka jamii moja kwenda jamii nyingine. Hata wakati baadhi ya tawala za nchi za Kikristu za Ulaya zilipokuwa katika kinachoitwa na baadhi ya wanahistoria kuwa ni Zama za Giza (Dark Ages) baada ya kuporomoka kwa utawala wa Kirumi na kupungua sana kwa upatikanaji wa maarifa nchi nyingine za Bara la Arabia zilikumbatia vitabu na elimu. Hii ni kweli kwani wakati Ulaya kunaporomoka katika maarifa nchi za Uarabuni za Kiislamu Mashariki ya Kati zilikuwa zinazama katika kukumbatia maarifa ambayo waliyapata kutoka katika vitabu vya Wagiriki wa kale. Hii iliendelea tena hadi ilipogeuka kwa mwamko tena wa Ulaya na kudidimia kwa nchi za Kiarabu nakuinka tena kwa nchi za Magharibi kuelekea kwenye karne ya 15. Njia kubwa ya kuhakikisha kuwa maarifa ya kila namna yanapatikana kwa urahisi na yanawafikia watu wengi ilikuwa ni kutengeneza mahali ambapo watu – wasomi na wasio wasomi – wangeweza kufikia vitabu na kusoma. Ndio maana hadi leo baadhi ya maktaba za kale kabisa bado zinafanya kazi huku nyingine zinakumbukwa tu kwa mchango wake. Maktaba za kale zinazojulikana ni pamoja na ile ya Alexandria (Misri) na ile ya Constantinople (Uturuki). Lakini pia zipo nyingine ambazo hazijapata umaarufu kama hizi na zinadumu ikiwemo ile ya Timbuktu (Mali) au zile za Chingueti (Mauritania).
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all