Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako
Kitabu cha Vijana Balehe
Kimeandikwa na Family Care International
sw
Kurasa 105
Kubalehe ni kipindi katika maisha ya wanadamu ambapo kijana anabadilika na kuwa mtu mzima. Kipindi hiki kina msisimko mkubwa, lakini pia ni kipindi chenye kuchanganya sana. Wakati wa kubalehe utaona mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia, pia unaweza kuwa na maswali mengi kuhusu mwili wako na uhusiano wako na wengine. Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya vijana balehe, ambao wana umri kati ya miaka 14 na 19 ili kiwasaidie kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokea wakati wa mabadiliko kutoka utoto kwenda utu uzima.Kitabu hiki kinatoa taarifa sahihi kuhusu mabadiliko yanayotokea katika kipindi cha balehe, pamoja na mambo mengine, kwa mfano: jinsi ya kuwa na afya njema ya kimwili na kihisia, kuepuka magonjwa yanayosababishwa na ngono zisizotakiwa, jinsi ya kupambana na misukumo ya kufanya ngono, na jinsi ya kujiepusha na matumizi mabaya ya vileo na dawa za kulevya. Pia, kitabu kinatoa ushauri kuhusu uhusiano mwema na wazazi, marafiki, wapenzi, jinsi ya kuweka malengo ya maisha, mbinu za kufaulu shuleni na maishani na jinsi ya kukabili vikwazo.
...
Kitabu cha Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako ni tafsiri ya “You, Your Life, Your Dreams” kilichoandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na shirika la “Family Care International” lenye Makao Makuu Mjini New York, nchini Marekani kwa kushirikiana na shirika la “Straight Talk Foundation” la Uganda. Toleo la awali kabisa liliandikwa na Catharine Watson Mkurugenzi Mhariri wa “Straight Talk Foundation” kwa kushirikiana na Ellen Brazier ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi wa Programu ya Afrika ya Mashariki katika Shirika la Ubora wa Afya kwa Familia Duniani. English translation: https://healtheducationresources.unesco.org/sites/default/files/resources/bie_fci_you_your_life_your_dreams_africa_602d_en.pdf
...
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.