Publisher Children's Radio Foundation
Childrens Radio Foundation (CRF) hivi sasa
hufundisha wanahabari vijana katika vituo
68 vya redio katika nchi sita za Afrika
(Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Liberia,
Ivory Coast , Afrika Kusini, Tanzania, na
Zambia) kutoa vipindi vya redio kila wiki na
shughuli za kijamii kila mwezi.
Unafanyia kazi mada kama vile mabadiliko
ya tabia nchi, afya ya kijinsia na uzazi, elimu,
uhamiaji, vurugu na usalama wa jamii, na
mengine. Unachukua wasikilizaji wa kipindi
cha redio na washiriki wa shughuli za
kijamii kwenye safari muhimu ya kuelewa
changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii
yako. Kwa kweli tunajivunia alama ambayo
umeiweka kupitia mazungumzo haya, na
tusingetaka hiyo isimame sasa.
Kuripoti kuhusu mada yoyote huhitaji
utunzaji na uwajibikaji, kutoa taarifa kuhusu
COVID-19 inahitaji hili zaidi.
Muongozo huu una malengo matatu makuu:
1. kuzingatia COVID-19 na kuipa
kipaumbele katika ajenda yako
2. kukujulisha kuhusu kuripoti na
kutangaza vipindi tokea nyumbani na
jinsi inavyofanywa
3. kukupa uwezo wa kupata vijana
wengine na watu wazima katika jamii
yako ambao wanataka kutoa hadithi/
simulizi zao za COVID-19
...