Rasta Kala Ndezi ni kijana aliyekosa dira tangu alipokuwa mdogo. Kazaliwa kutokana na mzazi mkatili na mlevi. Uhalifu ukawa kitu cha kawaida kwake, naye akawa mtu muafaka wa kutumika katika uhalifu.
Kala alipoingia katika biashara ya kuuza “mawe” akajikuta anaishi ndani ya mkondo wa Maisha ya kichinichini ya ufisadi uliokithiri.
Pesa za Mawe ni hadithi inayotufungulia pazia kutuonyesha yanayoweza kuwa yanatokea hivi sasa hapa Tanzania. Hadithi inatuchorea barabara ya biashara haramu ya madini inayovuka mipaka ya nchi, kanda na hatimaye kufika katika masoko makubwa ya dunia. Hadithi inatuonyesha jinsi maliasili yetu ya madini inavyoweza kuishia katika mikono ya watu wachache mno, watu ambao kwao “pesa” ni Imani, na ‘Ufisadi ‘ ni itikadi.
Cha kutia moyo ni kwamba Pesa za Mawe ni kielelezo kamili kuwa ufisadi haulipi.
...