Mchapishaji Mkuki na Nyota
Hiki ni kitabu cha Tatu katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli
vyenye mkusanyo wa hotuba za kila mwisho wa mwezi za Mheshimiwa
Rais Benjamin W. Mkapa anazotoa kwa Taifa.
Sambamba na kuendeleza falsafa yake ya “Uwazi na Ukweli”, Rais
Mkapa anaeleza na kufafanua kwa mapana na marefu masuala
mbalimbali yanayogusa maslahi ya Taifa katika maeneo kama vile:
• Utandawazi na Ushirikiano baina ya mataifa duniani;
• Demokrasia na wajibu wa viongozi wa mataifa mbalimbali kwa
wananchi wao;
• Usalama wa chakula na matatizo ya misaada kutoka mataifa
makubwa;
• Maendeleo na ufikiwaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia; na
Tathmini ya ubinafsishaji.
Pia anaeleza juu ya Mpango wa kurasmisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambao Rais anaamani utafungua
njia kwa makabwela kujipatia mikopo na mitaji ya kuanzishia na
kuendeshea miradi midogomidogo ya kujikimu kimaisha na hivyo
kupambana na umaskini.
Kitabu hiki kitawafaa Watanzania wote hasa wanapotaka kufuatilia
kwa karibu utendaji kazi wa serikali waliyoiweka madarakani. Ni
kumbukumbu muhimu kwa maendeleo ya Taifa na katika kuelewa
maswala ya siasa, jamii na uchumi wa jamii ya Tanzania.
...