You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Uwazi na Ukweli: Kitabu cha Tatu
Written by Benjamin W. Mkapa
Publisher Mkuki na Nyota
sw
Hiki ni kitabu cha Tatu katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli vyenye mkusanyo wa hotuba za kila mwisho wa mwezi za Mheshimiwa Rais Benjamin W. Mkapa anazotoa kwa Taifa. Sambamba na kuendeleza falsafa yake ya “Uwazi na Ukweli”, Rais Mkapa anaeleza na kufafanua kwa mapana na marefu masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya Taifa katika maeneo kama vile: • Utandawazi na Ushirikiano baina ya mataifa duniani; • Demokrasia na wajibu wa viongozi wa mataifa mbalimbali kwa wananchi wao; • Usalama wa chakula na matatizo ya misaada kutoka mataifa makubwa; • Maendeleo na ufikiwaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia; na Tathmini ya ubinafsishaji. Pia anaeleza juu ya Mpango wa kurasmisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambao Rais anaamani utafungua njia kwa makabwela kujipatia mikopo na mitaji ya kuanzishia na kuendeshea miradi midogomidogo ya kujikimu kimaisha na hivyo kupambana na umaskini. Kitabu hiki kitawafaa Watanzania wote hasa wanapotaka kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa serikali waliyoiweka madarakani. Ni kumbukumbu muhimu kwa maendeleo ya Taifa na katika kuelewa maswala ya siasa, jamii na uchumi wa jamii ya Tanzania.
...
link: https://mkukinanyota.com/product/uwazi-na-ukweli-3/
...
ISBN: 9789987417391
Thank you to Mkuki na Nyota
1 copy
Available for free in Arusha! Request
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all