You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Uwazi na Ukweli: Kitabu cha Kwanza
Raisi wa Watu Azungumza na Wananchi
Kimeandikwa na Benjamin W. Mkapa
Mchapishaji Mkuki na Nyota
sw
"Tangu mwanzo kabisa wa Serikali ya Awamu ya Tatu nilisema kuwa sera yangu ni Uwazi na Ukweli. Na niliwaambia viongozi wenzangu, kwenye Chama Cha Mapinduzi na kwenye Serikali, kuwa ni afadhali nichukiwe kwa kuwa mkweli, kuliko kupendwa kwa kuwa mwongo na mlaghai. Nilipotamka hivyo, wapo waliosema huo ni ushahidi kuwa mimi si mwanasiasa. Lakini nafurahi kuwa wananchi walinielewa, na wakaniamini. “Hotuba zangu za kila mwisho wa mwezi kwao ni mojawapo ya jitihada zangu za kuhakikisha wanajua Serikali inafanya nini, kwa sababu gani, na kwa faida gani kwao. Si haki kuwaongoza wananchi kwenda wasikokujua, au bila kuwaeleza sababu za kwenda huko. Serikali inayojiamini, na inayowajibika kwa wananchi, inakuwa wazi kwao. Haina sababu ya kujificha. Kiongozi aliyejiridhisha kuwa jambo fulani ni la manufaa kwa wananchi wake hana sababu za kuogopa kuwa mkweli, na kuelezea kwa nguvu ya hoja, kwa nini sera, mikakati na mambo fulani ni ya lazima. Ni vema, na haki, kuongoza walioelewa, kuliko kuongoza walioachwa gizani.” Hivyo ndivyo asemavyo, Mheshimiwa Rais Benjamin W. Mkapa katika utangulizi wa kitabu hiki cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vya hotuba zake za kila mwisho wa mwezi kwa wananchi. Hotuba hizo ni ufunguo wa uelewa sahihi wa siasa, uchumi na masuala ya jamii katika nchi yetu katika kipindi hiki cha historia. Umoja wa taifa, mshikamano na juhudi za maendeleo yanahitaji kipaumbele maalum katika dunia ya leo ya utandawazi, na Mheshimiwa Rais Mkapa anaeleza kwa ufasaha ni nini tunapaswa kufanya ili tuweze kufanikiwa.
...
ISBN: 9789987686438
Shukrani kwa Mkuki na Nyota
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all