Uwazi na Ukweli: Kitabu cha Kwanza
Raisi wa Watu Azungumza na Wananchi

Language: sw
Details: Categories: History, Language, Political economy & general, Politics, Swahili, University link: https://mkukinanyota.com/product/uwazi-na-ukweli-1/
Summary: "Tangu mwanzo kabisa wa Serikali ya Awamu ya Tatu nilisema kuwa sera yangu ni Uwazi na Ukweli. Na niliwaambia viongozi wenzangu, kwenye Chama Cha Mapinduzi na kwenye Serikali, kuwa ni afadhali nichukiwe kwa kuwa mkweli, kuliko kupendwa kwa kuwa mwongo na mlaghai. Nilipotamka hivyo, wapo waliosema huo ni ushahidi kuwa mimi si mwanasiasa. Lakini nafurahi kuwa wananchi walinielewa, na wakaniamini. “Hotuba zangu za kila mwisho wa mwezi kwao ni mojawapo ya jitihada zangu za kuhakikisha wanajua Serikali inafanya nini, kwa sababu gani, na kwa faida gani kwao. Si haki kuwaongoza wananchi kwenda wasikokujua, au bila kuwaeleza sababu za kwenda huko. Serikali inayojiamini, na inayowajibika kwa wananchi, inakuwa wazi kwao. Haina sababu ya kujificha. Kiongozi aliyejiridhisha kuwa jambo fulani ni la manufaa kwa wananchi wake hana sababu za kuogopa kuwa mkweli, na kuelezea kwa nguvu ya hoja, kwa nini sera, mikakati na mambo fulani ni ya lazima. Ni vema, na haki, kuongoza walioelewa, kuliko kuongoza walioachwa gizani.” Hivyo ndivyo asemavyo, Mheshimiwa Rais Benjamin W. Mkapa katika utangulizi wa kitabu hiki cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vya hotuba zake za kila mwisho wa mwezi kwa wananchi. Hotuba hizo ni ufunguo wa uelewa sahihi wa siasa, uchumi na masuala ya jamii katika nchi yetu katika kipindi hiki cha historia. Umoja wa taifa, mshikamano na juhudi za maendeleo yanahitaji kipaumbele maalum katika dunia ya leo ya utandawazi, na Mheshimiwa Rais Mkapa anaeleza kwa ufasaha ni nini tunapaswa kufanya ili tuweze kufanikiwa.