You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Uwazi na Ukweli: Kitabu cha Pili
Raisi wa Watu Azungumza na Wananchi
Kimeandikwa na Benjamin William Mkapa
Mchapishaji Mkuki na Nyota Publishers
Mwaka 2003
sw
Katika kitabu hiki cha pili kwenye mfululizo wa vitabu vinavyokusanya hotuba zake za kila mwisho wa mwezi (cha tatu kinaandaliwa), Rais Benjamin W. Mkapa anazungumzia matukio mema na mabaya ya mwaka 2002, pamoja na hatua za maendeleo zilizopigwa na taifa katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Rais Mkapa anaeleza kwa kina maana na athari za utandawazi kwetu kama taifa na kwa watu binafsi. Aidha anaendelea kueleza, kufafanua na kutetea sera ya ubinafsishaji na kuonyesha matunda ya sera hiyo bila kupuuza sokomoko kama ile iliyofuatia hatua ya kubinafsisha shirika la TANESCO. Rais Mkapa anaelezea vilevile masuala ya siasa, hasa utekelezaji mzuri wa MWAFAKA kati ya CCM na CUF kule Zanzibar ulioashiria utulivu wa kisiasa nchini na kurejesha upendo na mshikamano wa wananchi Visiwani. Kwa wale wote wanaopenda kufuatilia historia ya taifa letu, hotuba hizi za Rais Benjamini W. Mkapa ni kumbukumbu nzuri na ya kudumu ya miaka ya uongozi wake. Ni muhimu pia kwa viongozi, walimu na wanafunzi wa ngazi zote katika kuelewa na kuelezea masuala ya siasa, jamii na uchumi wa Tanzania.
...
link: https://mkukinanyota.com/product/uwazi-na-ukweli-2/ alternate isbn: 9987686435 9789987686438
...
ISBN: 9789987686766
Shukrani kwa Mkuki na Nyota Publishers
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all