You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Kusadikika
Nchi iliyo Angani
Kimeandikwa na Shaaban Robert
Mchapishaji Mkuki na Nyota
Mwaka 1991
sw
Kurasa 67
First published at the height of colonial occupation, this is an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. From the master of Swahili language and culture. Kwa zaidi ya miaka kumi na tano, vitabu vya mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na Kati, Marehemu Sheikh Shaaban Robert, havikupatikana Tanzania. Sababu ya kukosekana kwa vitabu hivyo ni kuwa kampuni ya kigeni iliyovichapisha iliamua kuacha kuvichapisha kwa sababu haikulipwa kwa fedha za kigeni jambo lililosabishwa na hali mbaya ya uchumi. Athari za kupotea kwa vitabu vya Sheikh Shaaban Robert katika miaka hiyo ni kwamba Watanzania wengi hasa wale wenye umri chini ya miaka thelathini, hawamjui mwandishi huyu maarufu na hawakulelewa katika mazingira ya utajiri wa maandishi yake ambayo bila shaka yoyote ni mfano pekee wa utajiri wa urithi wa utamaduni wetu. Kwa kuvichapisha vitabu vya Marehemu Sheikh Shaaban Robert, tunawakaribisha tena Watanzania, hasa vijana, kuvisoma, kuburudishwa na kufunzwa na yale aliyoyaandika kwa sanaa na kipaji adimu. First published at the height of colonial occupation, this is an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. From the master of Swahili language and culture. In Swahili. About the author Shaaban Robert is to the Swahili language what Shakespeare was to English. Acclaimed as the national poet, his publications have always been the touchstone of beauty of language, purity of spirit, and deep wisdom informed by African and Swahili culture in particular, but imbued with respect for and understanding of other cultures. Most prominent of his work is Kusadikika (To be believed), an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. Published at the height of colonial occupation in Tanzania. Shaaban Robert kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza. Akikubalika kama msahiri wa taifa, vitabu vyake daima vimekuwa kipimo cha juu cha uhondo wa lugha, usafi wa nia na hekima kutokana na utamaduni hususan wa Kiafrika na Waswahili lakini pia kwa jnsi alivyoelewa na kusheshimu tamadui nyingine. Katika vitabu vyake Kusadikika ndicho maarufu kushinda vyote. Hii ni hadithi ya kiistara juu ya nchi ambako dhulma inatawala kinyume na haki, sheria na utu. Kitabu kilichapishwa wakati ukoloni umetanda nchini Tanzania.
...
ISBN: 9976973101
Shukrani kwa Mkuki na Nyota
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all