You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Mwanangu Rudi Nyumbani
Kimeandikwa na Dotto Rangimoto
Mchapishaji Mkuki na Nyota
Mwaka 2018
sw
Kurasa 94
Muswada huu umesomwa na majaji watatu: Ken Waribora Waliaula (Mwenyekiti wa Majaji), mwanataaluma na mwandishi; Daulat Abdalla Said, mwanataaluma na mwandishi, anayesomesha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar; na Ali Attas, mwandishi na mwalimu wa Kiswahili na Kiingereza, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Japan. Wakizingatia historia ndefu ya uandishi katika lugha ya Kiswahili, majaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika wameeleza: Mashairi yaliyomo katika diwani hii yametumia lugha iliyojaa taswira na majazanda yanayowakilisha vyema hisia zinazoelezwa katika dhamira mbalimbali. Mshairi amefaulu sana kuzitumia mbinu na miundo kadha wa kadha ili kuyajadili maswala yanayohusu hali na mazingira tafauti tafauti katika maisha ya binadamu. Anayazungumza maswala mazito mazito, lakini kwa namna ambayo hayamuelemei msomaji wake. Badala yake, huwa yanamhimiza aendelee kuyasoma. Hata yale maswala makongwe, kwa mfano uhusiano baina ya wazazi na wana wao, yanajadiliwa kwa namna ya kuvutia na kuyafanya kana kwamba ndiyo mwanzo, yanaanza kujadiliwa sasa. Dotto Rangimoto ni mtunzi stadi. Na diwani hii ni mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili wa zama zetu hizi. Selected from 30 entries, the manuscripts were read by 3 judges: Ken Walibora Waliaula, the Judge Chair, scholar and writer, Daulat Abdalla Said, Assistant Lecturer at the State University of Zanzibar (SUZA), and Ali Attas, Kiswahili and English teacher at the Ministry of Foreign Affairs, Japan. “In Mwanangu Rudi Nyumbani one encounters seductive metaphors and imagery, effectively and successfully used in diverse Kiswahili poetic forms and styles while articulating concerns that have direct bearing to the human condition. Dotto discusses weighty and serious matters but in a manner that doesn’t burden the reader. Instead he encourages one to keep on reading. He is a master of the craft. The volume is a great contribution to contemporary Kiswahili poetry.” – The judges, in recognizing the long Kiswahili literary tradition
...
link: https://mkukinanyota.com/product/mwanangu-rudi-nyumbani/
...
ISBN: 9987083749
Shukrani kwa Mkuki na Nyota
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all