Mchapishaji Mkuki na Nyota Publishers
Hiki ni kitabu cha Nne katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli
vyenye mkusanyo wa hotuba za kila mwisho wa mwezi za Mheshimiwa Rais
wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,
Benjamin W. Mkapa.
Katika Toleo hili Rais anajadili kwa uwazi na ukweli juu ya masuala mbalii
mbali ya muhimu kwa taifa, kama vile:
Ulazima wa kuweka Bajeti Ndogo ili kugharimia athari za ukame
kama vile uhaba wa chakula na ugharimikiaji uzalishaji wa
umeme; pia gharama za uandaaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura;
Ripoti ya Tume ya Kimataifa kuhusu Masuala ya kijamii katika
Utandawazi na umuhimu wa kufanya juhudi za kuepuka athari za
utandawazi kuanzia nyumbani;
Ushirikiano wa utatu kati ya Serikali, wananchi na wahisani katika
kupiga vita umaskini;
Umuhimu wa kushiriki katika Tume ya Kimataifa iliyoanzishwa na
Mheshimiwa Tony Blair, Waziri Mkuu wa Uingereza;
Dhana halisi ya Bajeti ya Taifa na namna dhana hiyo inavyotakiwa
kueleweka; na
Dhima ya wananchi na Serikali katika vita dhidi ya ugonjwa waPia mheshimiwa Rais anazungumzia umuhimu wa wananchi katika kushiriki-
ana na jeshi la polisi ili kupunguza wimbi la uhalifu. Anaeleza pia uanzishaji
wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kufuatia mafani-
kio makubwa ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya msingi (MMEM)
hatimaye anaeleza kuhusu Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
Tanzania (MKURABITA), hali ya siasa nchini na uhusiano na ushirikiano na
mataifa ya nje.
...