Historia ya Klabu ya Simba
1920-2014
Kimeandikwa na Mwina Kaduguda
Mchapishaji Mkuki na Nyota Publishers Limited
Mwaka 2014
sw
Kurasa 128
History of Simba soccer club. Hiki ni kitabu cha kwanza chenye historia ya kina ya Simba Sports Club. Kama mpenzi wa soka, hususan mkereketwa wa Simba, utajua chimbuko na undani wake tangu ilipoanzishwa hadi hii leo. Vilevile utaweza kutumia kitabu hiki kama ushahidi katika mabishano na mijadala inayohusiana na klabu. Utasoma vioja vya soka letu kama vile ushabiki wa kupindukia, vituko na imani za kishirikina, makundi yaliyotia fora, migogoro, mafanikio, picha za matukio mbalimbali, bila kusahau rekodi za mwenendo wa timu na misimamo ya ligi katika historia ya klabu. Kwa kukisoma kitabu hiki utafahamu pia mambo mengi yanayolizunguka soka la Tanzania, kwani rekodi hizi hazipatikani kwa urahisi na mwandishi ametumia muda mwingi kufanya utafiti na kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali rasmi kama vile maktaba, vitabu, magazeti, nyaraka na kuwahoji wazee wa zamani. Kwa mfano, utajua ni lini soka liliingia na kusambaa nchini katika karne ya 20, mpasuko uliozaa Simba na Yanga na mengine mengi ya kuburudisha, kuelimisha na kusisimua.
...
ISBN: 9987081630
Shukrani kwa Mkuki na Nyota Publishers Limited
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.