Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Kisiki Kikavu
Kimeandikwa na Aldin Kaizilege Mutembei
Mchapishaji E & D Vision
Mwaka 2005
Kurasa 72
Kalabweli alitarajia kuwa angewatunza wazazi wake,dada na wadogo zake.Na kwa kweli kalabweli alifanikiwa katika biashara,akashamiri,akapenda na kupendwa,akaijua pesa……….. Kisiki kikavu kinatufunulia maisha ya Kalabweli ambayo yamebeba historia ya UKIMWI huko mkoani Kagera.Historia iliyoanzia katika umasikini uliofuatia vita vya Iddi Amin,hali iliyozaa biashara ya magendo na maisha ya starehe iliyokithiri.UKIMWI ukabisha hodi ukapatiwa majina;Juliana,Silimu;Ninja………… Kisiki Kikavu kinaweka wazi udhaifu wetu katika kukabili changamoto za maisha.Jinsi unavyozidi kusoma kisiki Kikavu ndivyo unavyoona kwamba historia,siasa,mila na uchumi vimeshikamana katika kuibua na kutandawaza janga la UKIMWI,na hapo unagundua ukavu wa fikra za mwanadamu. Hii ni riwaya ya aina yake inayochambua taathira za vvu,uelewa wa watu,ukubalifu wao na jinsi tabia zinavyobadilika kwa wakati ,na kwa rika .Ni riwaya ninayopendekeza isomwe na kila mmoja anayetaka kujua undani changamoto inayotukabili kuhusu UKIMWI Profesa F.E.M.K Senkoro, Mwanafasihi na Mkuu wa Idara ya Kiswahili , Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
...
link: https://vitabu.edvisionpublishing.co.tz/product/kiski-kikavu/ Fiction
...
ISBN: 9987411347
Shukrani kwa E & D Vision
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.