You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Mwongozo kwa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano
Toleo la 3
Publisher Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority - TCRA)
Published 2019
sw
Pages 65
Download
1.5 MB
Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia kukua kwa kasi kwa sekta ya Mawasiliano hapa nchini na duniani kwa ujumla. Kumekuwa na ongezeko la huduma zinazowezeshwa na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Fursa zinazotokana na kuongezeka huku na pia idadi ya watumiaji na watoa huduma imeongezeka. Mabadiliko katika sekta ya mawasiliano yameleta maendeleo makubwa na kurahisisha na kubadili kwa kiasi kikubwa namna ambavyo tunafanya shughuli zetu mbalimbali. Pamoja na mchango huu mkubwa na wenye kuongeza tija katika shughuli zetu, maendeleo haya pia yamekuja na changamoto mbalimbali zikiwemo za kitamaduni, maudhui na staha, kiusalama, masuala mapya na wakati mwingine hali ya sintofahamu kwa upande wa watumiaji wa huduma hizi. Mwongozo huu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano wa mwaka 2019 ni toleo la tatu na umeboreshwa kwa kuzingatia mabadiliko ya sheria na Kanuni mpya ambazo hazikuwepo wakati wa uchapishaji wa toleo la kwanza la mwaka 2017. Mwongozo huu umezingatia mabadiliko yaliyopo sasa kwenye sekta ya mawasiliano na utakuwa unachapishwa mara kwa mara kwa kuzingatia mabadiliko katika teknolojia na maendeleo ya sekta kwa lengo la kuwaonyesha watumiaji utaratibu bora wa kufuata ili kufaidi huduma za mawasiliano ambazo wamezilipia au wamewezeshwa kuzitumia, ili kupunguza na pale inapowezekana kuondoa kabisa changamoto ambazo zinaweza kuwaletea athari hasi katika matumizi ya huduma na bidhaa za Mawasiliano. Mwongozo huu pia umekusudiwa kumwezesha mtumiaji wa huduma za Mawasiliano kujilinda dhidi ya matukio yanayoweza kutokea na kumsababishia athari za kiafya, kiusalama au upotevu wa mali zake. Mwongozo umefafanua dhana mbalimbali, umewachambua wadau wa sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania pamoja na kazi zao, umeainisha majukumu na kazi za mdhibiti wa sekta hii kwenye kumlinda mtumiaji na umeelezea haki na wajibu wa watumiaji. Vilevile Mwongozo huu una lengo la kutoa dondoo muhimu kwa wanaotumia huduma za simu na intaneti, huduma za utangazaji na huduma za posta. Katika Mwongozo huu mtumiaji atapata pia ufahamu kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko pale ambapo haki yake imekiukwa au pale ambapo hakupokea huduma kwa kiwango ambacho mtoa huduma aliahidi kufanya hivyo. Mtumiaji pia atafahamishwa kanuni zinazomlinda, masuala mtambuka na tahadhari na mambo ya kuzingatia anapotumia huduma na bidhaa za mawasiliano. Ni matarajio yetu kuwa Mwongozo huu utakuwa msaada mkubwa kwa walengwa ili kuwawezesha kupata thamani halisi ya fedha zao, na pia kufurahia na kufaidi fursa zilizopo katika matumizi ya TEHAMA.
...
Thank you to Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority - TCRA)
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all