You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Kiswahili - Mazoezi ya Lugha - Kitabu cha Mwanafunzi - Darasa la 1
Mchapishaji RTI, Jamhuri ya Kenya, USAID
Mwaka 2021
sw
Kurasa 153
Pakua
18.1 MB
Kimeidhinishwa na KICD - Kimeainishwa kwa mtaala uliojikita kwenye ufarisi. Kitabu hiki kinaendana na kiongozi cha mwalimu. Kitabu hiki cha Kiswahili Mazoezi ya Lugha kwa gredi ya 1 hutumia mbinu mwafaka iliyofanyiwa utafiti wa hali ya juu iii kumsaidia mwanafunzi kukuza umilisi wa stadi za lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kimezingatia Umilisi wa kimsingi, uhusiano na masuala mtambuko na stadi nne kuu za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Zaidi ya haya, kitabu hiki kimezingatia pia mada zote na maadili yaliyopendekezwa katika mtalaa mpya wa kitaifa. Kitabu hiki kitawapa wanafunzi wa gredi ya 1 fursa ya kujifunza kutokana na tajriba mbalimbali na tathmini ambazo humwezesha mwanafunzi kuonyesha umil i si wa kimsingi unaotarajiwa katika lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kimeegemea na kuzingatia tajriba zinazotokana na mradi wa Wizara ya Elimu unaoitwa Tusome. Mradi huu wa Tusome umefadhiliwa na USAID. lnatarajiwa ya kwamba mwanafunzi atakayekamilisha yaliyomo kwenye kitabu hiki atakuwa na umilisi wa stadi za lugha ya Kiswahili kama vile: kusoma kwa ufasaha na kwa mtiririko ufaao na umilisi wa kuandika. Baadhi ya sifa maalum za kitabu hiki cha gredi ya 1 ni kama zifuatazo: - Shughuli za kuchangamsha zinazotumiwa kufundishia mada za mtaala wa Kitaifa. - Kazi imepangwa katika mfumo maalum wa kimantiki. - Picha na michoro inayoambatana na hadithi zilizomo na tajriba za mwanafunzi. - Hadithi za kusisimua zinazonuia kuendeleza stadi na umilisi wa lugha ya Kiswahili. - Hadithi katika tanzu mbalimbali zinazomwezesha mwanafunzi kujisomea. - lnsha za kuongozwa zinazomwezesha mwanafunzi kukuza stadi ya kuandika. - Hadithi za mwalimu zinazomwezesha mwanafunzi kukuza stadi ya kuzungumza na kusikiliza kwa makini. Kitabu hiki kiliandaliwa na wataalam kutoka Wizara ya Elimu (MOE), Turne ya Kuwaajiri Walimu (TSC), Taasisi ya Usimamizi wa Elimu ya Kenya (KEMI), Taasisi ya Elimu ya Mahitaji Maalum ya Kenya (KISE).
...
Kitabu hiki cha mwanafunzi kinatumika pamoja na Mwongozo wa Mwalimu
...
ISBN: 9789966110084
Shukrani kwa RTI, Jamhuri ya Kenya, USAID
Create an account to...
View comments and discuss this book!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all