You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu
Toleo la Pili
Publisher East and Horn of Africa Human Rights Defenders Project
Published 2012
sw
Pages 78
Download
1.7 MB

Miaka mitano imepita tangu Mradi wa Watetezi wa Haki za Binadamu Afrika ya Mashariki na Pembe ya Afrika ulipochapisha toleo la kwanza la Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Rejea kwa Watetezi wa Haki za Binadamu. Baada ya hapo changamoto mpya zimeendelea kukua na kutengeneza mazingira ambayo watetezi wa haki za binadamu wanafanyia kazi.

Nchi mbalimbali zinaendelea kutumia sheria zenye vikwazo vinavyozuia uhuru wa kuendesha kazi ya haki za binadamu. Hatua dhidi ya vitisho zilizofikiria zaidi kuimarisha utekelezaji wa sheria ya uhuru wa kuamua na kutumia mabavu, pamoja na kupitiwa kwa mahakama katika upunguzaji uzito au ucheleweshaji wa kesi zinazidi kutumika ili kuzuia mbinu halali za uchunguzi na upinzani kutoka kwa watendaji wa asasi za kiraia. Ushirikiano na nchi za nje ina maana watetezi wa haki za binadamu waliolazimishwa kuingia kizuizini wanaweza kuendelea kunyanyasika hata katika nchi zao za hifadhi. Sheria zisizothibitishwa kwa ajili ya asasi zisizo za kiserikali zimekuwa zikitumika katika baadhi ya kesi, kuzuia fursa za fedha na pia shughuli za haki za binadamu, wakati sheria za vyombo vya habari mara nyingi hutafsiriwa na kutumiwa kiholela na kunyima uhuru wa kujieleza. Watetezi wa kundi la wachache katika mwenendo wa kufanya mapenzi wanaendelea kupigania wapate kutambuliwakwamba haki za wasagaji, mashoga, wanaovutiwa kimapenzi na watu wa jinsia zote mbili, wenye jinsi mbili na wa jinsi tata ni haki za binadamu, wakati vitisho kutoka kwa watendaji wa serikali na wasio wa serikali vimejenga pengo la uhasama kwa watetezi hawa.

Wakati changamoto hizi zinabadilika, nyenzo ambazo zipo kwa ajili ya watetezi wa haki za binadamu pia zimeendelezwa na kuwa za kisasa na za ufanisi zaidi. Matumizi kamili ya nyenzo hizi kwa njia ya kimkakati ni changamoto na uwezekano wa kuwapa nguvu watetezi madhubuti wa haki za binadamu.

Kujihusisha na mifumo ya kimataifa na kikanda ya haki za binadamu ni moja ya njia bora zaidi za kujenga utumbuzi wa masuala ya haki za binadamu na hata kuhitaji wadau wabeba majukumu kushughulika rasmi. Sura ya 1 ina mjadala wa njia hizi na matumizi yake ya ufanisi.

Matunzo binafsi na usalama wa kitaalamu kwa watetezi wa haki za binadamu ni muhimu ili juhudi zao ziwe endelevu. Sura ya 2 na 3 zinahusu usimamizi wa usalama na kupunguza mfadhaiko kwa watetezi wa haki za binadamu kwa mtiririko huo.

Mikakati kwa ajili ya kuendesha kampeni inajadiliwa katika Sura ya 4, ambayo imerekebishwa kwa majadiliano ya nyenzo za vyombo vya habari vya kijamii kwa ajili ya kufikia malengo ya utetezi katika Sura ya 4.5.

Changamoto na mikakati maalum ya kutetea haki za wanawake na haki za kundi la wachache katika tabia ya mwenendo wa kufanya mapenzi zinashughulikiwa katika Sura ya 5 na 6 kwa mtiririko huo.

Hatimaye viambatanisho vya rejea vimerekebishwa kujumuisha machapisho yanayohusiana zaidi na mashirika yanayoshughulika na watetezi wa haki za binadamu.

Tumefurahi kuweza kufanikisha kitabu hiki kupatikana kwa Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kiswahili, Kiamhari, na Kisomalia, hivyo kufanya kiwafikie watu wengi katika kanda hii.

Tunamshukuru mfadhili wetu mkuu katika mradi huu, Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la Uswidi.

Mradi wa watetezi wa Haki za Binadamu Afrika ya Mashariki na Pembe ya Afrika unawashukuru kwa dhati wote waliochangia kitabu hiki cha rejea kwa maoni yao, hali kadhalika kwa kazi yao endelevu katika huduma ya haki za binadamu.

Mradi wa watetezi wa Haki za Binadamu Afrika ya Mashariki na Pembe ya Afrika unatoa kitabu hiki kwa heshima ya wale wote waliopoteza maisha yao katika kupigania haki za binadamu. Tuungane katika kujenga maisha bora ya baadaye

...
Kitabu hiki kinapatikana katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kiamhari, Kiswahili, na Kisomali hapa. Toleo la kwanza lilitayarishwa na Norah Rehmer Toleo la pili limetayarishwa na Neil Blazevic
...
Thank you to East and Horn of Africa Human Rights Defenders Project
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all