You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

View this book in English Living Safely with Bats
Kuishi Salama na Popo
Kimeandikwa na
Mchapishaji EcoHealth Alliance
Mwaka 2019
sw
Kurasa 51
Pakua 34.1 MB
katika kitabu hiki utajifunza: * Kwamba popo wana umuhimu katika mazingira yanayotunzunguka * Njia za kuishi salama na popo * Njisi ya kutupa popo waliokufa * Jinsi ya kufanya kama kutoishi na popo hai ni vigumu * Jinsi ya kudhibiti popo kwenye makazi * Njia za kudhibiti popo waliopo nje makazi yako Popo ni sehemu muhimu ya mazingira yetu. Popo wanafanya majukumu makubwa ya kututunza watu na kuweka mazingira salama kwa mfano, kusambaza mbegu za miti ya mbao na matunda. Popo pia wanakula wadudu mbali mbali wanaoharibu mazao. Wakati popo wanasemekana kuwa na virusi vya kichaa cha mbwa na magonjwa mengine, kitendo cha kuwaua au kuwasumbua kwenye makazi yao ya asili kinaweza kusababisha kusambaa zaidi kwa virusi vya kichaa cha mbwa kwa watu wengi zaidi. Kwa sababu hii ni vyema kutokuwaua, kuwawinda, kuuza, kupika au kuwala popo. Njia bora ya kuishi salama na popo ni kuepuka kuwa karibu na popo hai au waliokufa. Ni muhimu sana kuepuka vitu kama kugusa mate, damu, mikojo na vinyesi vyao na kutengeneza mazingira yasiyo ruhusu wao kuishi ndani ya nyumba na majengo yetu.
...
Shukrani kwa EcoHealth Alliance, USAID
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all