Roho Mtakatifu na Maisha Mapya
Published Year: 1984
Language: sw
Details: Mwandishi wa Kitabu hiki, Mch. Dr. Norvald Yri ni profesa wa Theologia ya Biblia katika chuo cha Theologia Makumira, Tanzania. Amejaribu dukuduku nyingi za wakristo kuhusu Roho Mtakatifu, uamsho, kuongozwa na kuendesha katika Roho, karama za Roho, na kadhalika. Kitabu hiki kinafaa kama kitabu cha kurejea (textbook) katika shule za Sekondari na vyuo mbalimbali vya Biblia, na hasa sharikani na mahali ambapo Biblia inasomwa.
Summary: Je, unayafahamu mambo ya Roho Mtakatifu? Je, ninaye Roho Mtakatifu? Je nimebatizwa na Roho? Maswali kama haya yanaulizwa mara kwa mara, hasa na vijana. Ni rahisi kujichunguza wenyewe na mioyo yetu ili kujaribu kujua juu ya mambo ya aisha ya kiroho. Sijaeleza kila jambo juu ya Roho Mtakatifu na Yesu Kristo. Tumepata habari juu ya kuja kwake. Siku hizi tunasikia habari tofauti juu ya Roho Mtakatifu na huduma yake, hata sio rahisi kujua jambo lipi ni la kweli au la uongo. Je wakristo wote wamepata karama za kiroho, au la? Nafikiri umesikia wale ambao wanakaza "kunena kwa lugha," matendo ya miujiza na kadh., kuwa karama za kiroho muhimu zaidi kuliko zote zingine. Tunaposoma Agano jipya, tunaona msimamo huu kuwa ni wa Neno la Mungu? Nataka kwa neema ya Mungu, kuyaeleza mambo ya Roho Mtakatifu kwa msingi wa ufuno wa Mungu katika Biblia. Lengo langu pia ni kwamba watu wengi wafahamu maana ya maisha mapya ya Kikristo.