Publisher University of Maryland Extension
Kuku wanapatikana duniani kote, na wanabadilisha chakula chao kuwa kuwa nyama kwa ufanisi. Protini bora ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mtoto. Kuboresha ufugaji wa kuku sio tu huongeza usalama wa chakula na lishe, bali pia ni kuongeza uhakika wa kipato.
Wastani wa matumizi ya nyama ya kuku duniani ni takribani kilo 13.2 kwa kila mtu kwa mwaka. Wastani wa matumizi ya mayai duniani ni takribani kilo 8.9 kwa mtu kwa mwaka.
Kuku wa kisasa wanaweza kufikia uzito unaokubalika kwenye soko ndani ya miezi 3.
Kuku anaweza kutaga mayai 300 kwa mwaka.
Kwa sababu gharama za kuanzisha na kuendesha zipo chini, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuboresha maisha ya watu, ufugaji wa kuku ni moja ya sehemu ya kuanzia katika biashara za kilimo duniani
...