Sign up for news and free books by email!
Mwongozo wa Muundo na Utendaji Kazi wa Kamati za Shule za Msingi
2016
Pages 70
Publisher: EQUIP-Tanzania sw
Maendeleo ya taifa lolote yanategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa elimu ya watu wake. Mahitaji ya utoaji wa elimu bora na usimamizi unahitaji uwajibikaji wa karibu kutoka ngazi ya Taifa, Mkoa, Halmashauri na Serikali ya Kijiji/ Mtaa. Ugatuaji wa madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Mamlaka ya Serikali ya Kijiji/Mtaa imekasimu madaraka ya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Shule kwa Kamati za Shule. Elimu ni nyenzo muhimu katika kupambana na maadui Ujinga, Maradhi na Umaskini miongoni mwa jamii. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sera ya Elimu na Mafunzo, Dira ya Taifa ya Maendeleo na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) vyote vinaipa elimu nafasi ya pekee na kipaumbele katika kuboresha maisha ya Watanzania wote bila kujali jinsi, rangi, kabila au dini ya mtu. Ili kufikia ufanisi unaotarajiwa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakishirikiana na Wakala wa Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) na Washirika wa Maendeleo ya Elimu - GPE kupitia mradi wa LANES wameweka mikakati mbalimbali ya kujenga uwezo na kuimarisha utendaji wa kamati ya shule. Ili kufanikisha lengo hili, mwongozo huu umeandaliwa kutoa maelekezo ya kuunda Kamati za Shule na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Madhumuni ya mafunzo ya Uimarishaji wa Uwezo wa Kamati za Shule ni kuwaelewesha wajumbe juu ya kazi na wajibu wao katika kusimamia maendeleo ya shule. Pia kuwapa nyenzo za kufanyia kazi kwa kuwapatia miongozo mbalimbali, Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali za Serikali juu ya elimu nchini. Mwisho tunachukua fursa hii kuwatakia mafunzo mema wale wote watakaopata mafunzo ya kitaifa ya Uimarishaji wa utendaji kazi wa Kamati za Shule.
...
ISBN: 9789987458196
Thank you to Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu, EQUIP-Tanzania
Download free pdfs
Free books by category
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all