You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Uchakataji Ngozi Kwa Kuzingatia Utunzaji wa Mazingira
Mafunzo Yanayohusu Mbinu Na Usimamizi wa Uchakataji Mdogo
Written by Jaap Kok
Publisher USAID
sw
Download 2.2 MB
Kitabu hiki kimelenga watu wenye nia ya kuanzisha uchakataji mdogo wa ngozi. Pia kwa wale wanaopata ugumuwa kuanza kwa kutumia ujuzi walioupata kwa kusoma vitabu vingine vya nadharia. Vitabu ambavyo huenda vinaelezea mbinu za juu zaidi za Uchakataji, Mbinu ambazo zinatumika katika viwanda vikubwa kama vile mashine, bidhaa za kemikali na uwekezaji mkubwa. Kitabu hiki kimekusudiwa kuwa mwongozo kwa vitendo, kwa wale wanaotaka kuchakata ngozi kwa idadi ndogo kuanzia ngozi tanohadi kumi za mbuzi ambazo huweza kupatikana katika machinjio kila wiki. Pia kimezingatia upatikanaji wa vifaa, zana na uwekezaji mdogo katika vijiji na maeneo ya jirani. Katika kitabu hiki neno Vitendo litakuwa la muhimu sana kuliko neno la kisayansi. Hata hivyo kitabu kitatoa maelezo ya awali kuhusiana nahatua zinazohusika katika mchakato wa kubadilisha ngozi na kuwa ngozi iliyochakatwa. (Ngozi iliyotayari kutengenezea bidhaa). Katika sura nne za mwanzo tutajadili nadharia. Tunafikiri msomaji anahitaji kuwa na ufahamu wa nadharia kwa muhtasari ili aweze kuelewa mchakato wa Uchakataji. Sura ziizobaki huelezea Uchakatajikwa vitendo. Tunaelezea Uchakatajiwa ngozi ya mbuzi kwasababu ni rahisi kuimudu na zina vipimo vidogo. Ngozi iliyochakatuliwa (ngozi iliyotayari kufanyiwa kazi) inaweza kutumika kwa kutengenezea bidhaa mbali mbali. Na pale mtu akijua kutengeneza ngozi yake mwenyewe atapata urahisiwakutengeneza aina nyingine za ngozi, kwani kanuni zote za Uchakataji zinafanana.
...
Transfer of Technology for Development - Amsterdam Environmentally-friendly leather making
...
Thank you to USAID
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all