Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Mbinu za Ujifunzaji kwa Wote
Mbinu za Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Walimu wa Shule za Msingi na Madarasa ya Awali kwa Kuzingatia Mfumo wa Elimu Jumuishi
Kimeandikwa na Tusome Pamoja
Mchapishaji USAID, TET
Mwaka 2020
sw
Matini hii inaongozwa na misingi ifuatayo: • Watoto wote wana uwezo wa kujifunza. • Wanafunzi wanaweza kupata changamoto za kujifunza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutoifahamu vyema lugha ya kufundishia, ugonjwa, njaa, hofu, kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji/ukatili nyumbani na mashuleni, kuwa na ulemavu na mengineyo ambayo hayajabainishwa hapa. • Si wakati wote unaweza kutambua kama mtu ana ulemavu kwa kumwangalia tu. • Usimwandike mtoto kama mwenye ulemavu, bali bainisha vifaa na mahitaji yanayoweza kutumika kumsaidia mtoto huyo kujifunza. Elimu Jumuishi ni nini? Ili kuzielewa mbinu jumuishi za ufundishaji na ujifunzaji katika elimu jumuishi, ni muhimu kwanza kuelewa maana ya elimu jumuishi. Elimu jumuishi inamaanisha kuwaelimisha wanafunzi wote, kulingana na mahitaji yao katika darasa moja...
...
Shukrani kwa USAID, TET
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.