Mwongozo wa Mafunzo ya Kuimarisha Kusoma katika Mtaala

Faster download
Download 1.1 MB

Published Year: 2015

Book Thumbnail

Language: sw

Details: Mafunzo haya ya Kuimarisha Usomaji katika Mtaala kwa walimu wa darasa 3 na 4 ni matokeo ya msaada wa watu wa Amerika kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada ya Kimataifa ya Mendeleo la Marekani (USAID) kwa Programu ya Elimu ya Msingi ya TZ21. Msaada huu wa watu wa Marekani unalenga kujenga uwezo wa watoto wa Tanzania kielimu. Msaada huu unakusudia kuboresha stadi za usomaji za wanafunzi katika hatua za awali wanapoanza kusoma shuleni ili kuinua matokeo mazuri ya usomaji yanayotarajiwa kwa watoto wote wa shule

Summary: Walimu waweze: 1. Kutafakari kuhusu maendeleo na changamoto za kusoma, kuandika na kutumia msamiati kujifunza maudhui ya masomo mengine darasani. 2. Kujifunza zaidi jinsi ya kupambana na changamoto za ufundishaji zinazowakabili. 3. Kujifunza na kufanyia mazoezi mbinu mpya za kusoma, kuandika na kutumia msamiati katika kujifunza maudhui ya masomo mengine. 4. Kuchunguza dhana ya matini inayoendana na ngazi/uwezo wa msomaji. 5. Kuandika matini mpya za kufundishia katika ngazi mbalimbali kulingana na mahitaji tofauti tofauti ya kujifunza. 6. Kutumia matini mpya kuandaa masomo ya kufundisha maudhui kwa kutumia mbinu za kusoma, kuandika na msamiati.