Sign up for news and free books by email!
Mtindo wa Maisha na Magonjwa yasio ya Kuambukiza
2013
Dalili, Athari na Kinga - Elimu kwa Jamii (LIfestyle and Noncontagious Diseases - symptoms, effects and prevention - Community Education)
Publisher: Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Kisukari Tanzania sw
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, maradhi yanayohusiana na upumuaji na saratani yanazidi kuongezeka kwa kasi na yanaendelea kuwa chanzo kikuu cha vifo duniani kote. Inakadiriwa Kisukari pekee kimeathiri maisha ya watu takriban 371 milioni duniani kote, huku 80% ya idadi hiyo ikiishi katika nchi zenye uchumi wa kati na nchi masikini. Kwa upande wa Tanzania, takriban watu wazima 9 kati ya 100 wana ugonjwa wa kisukari, na mtu mzima 1 kati ya 3 ana tatizo la shinikizo la juu la damu. Gharama ya kukabiliana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani kote ni mabilioni ya dola na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa rasilimali finyu zilizopo. Kwa mwaka 2010 Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa jumla ya gharama za huduma za afya zinazohusiana na kisukari zilifikia dola 378 bilioni duniani kote, na kiasi hiki cha fedha kinaweza kufikia dola 490 bilioni ifikapo mwaka 2030. Nchi zinazoendelea kama vile Tanzania (na hata nchi zilizoendelea pia) hazina rasilimali za kutosha kutibu watu wote wanaobainika kuwa na kisukari. Hivyo, jitihada za kukabiliana na tatizo hili ni budi zikajikita zaidi katika mitazamo jumuishi inayolenga kukinga ili kupunguza kiwango cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye jamii yetu. Kwa kufahamu hili Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Kisukari Tanzania, pamoja na wadau wengine ilitayarisha Kijitabu hiki kwa jamii kwa lengo la kupunguza athari na matokeo mapya ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye jamii ya Watanzania. Kijitabu hiki kimeandikwa kwa lugha nyepesi na kinajumuisha taarifa muhimu na kinampa nafasi kila mtu kuchagua mtindo wa maisha utakaomwezesha kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa usioambukiza. Tunawaasa watu wote kusoma Kijitabu hiki, na hatimaye kutoa mchango wao katika kuboresha afya.
...
Thank you to Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Kisukari Tanzania
Not part of any reading lists yet
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Or check out these books being discussed
Books being discussed
Related books: Browse all