Sign up for news and free books by email!
Ukweli Kuhusu Maisha
Written by Shirika la Afya Duniani
Publisher: World Health Organization sw
Tangu toleo la kwanza litolewe miaka mitatu iliyopita, kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha kimekubalika duniani kote. Zaidi ya nchi 100 zimetoa tafsiri ya kitabu hiki na hivi sasa zinatumika zaidi ya nakala milioni nane katika lugha 170. Wito ulio katika kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha ni rahisi. Waganga wengi wanakubaliana na habari za kimsingi zinazohusu afya ya watoto ambazo familia zote zina haki ya kuzifahamu. Kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha kimeweka h abari zote hizo pamoja. Ni maelezo yenye uhakika, yaliyo katika lugha nyepesi ambayo taaluma ya tiba mayafahamu kuhusu njia rahisi na za gharama nafuu za kulinda uhai na afya ya watoto. · - Ni maelezo ambayo yatasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watoto katika nchi zinazoendelea. - Ni maelezo ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa k upunguza matatizo ya utapiamlo, kulinda afya na ukuaji bora wa kizazi kijacho. - Ni maelezo ambayo karibu wazazi wote wataweza kutekeleza kwa kiwango fulani kwa gharama nafuu. Kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha kimetolewa kwa pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) , na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Kushugulikia Idadi ya Watu (UNFPA) wakishirikiana na mashirika mengine zaidi ya 160 ya kuhudumia watoto yanayofahamika sana duniani. Wanamawasiliano Kila juma, watoto robo milioni hufa katika nchi zinazoendelea. (Nchini Tanzania watoto wapatao 4,500 hufa kila juma). Mamilioni ya watoto wengin e htiishi na afya mbaya na ukuaji duni. Sababu ya kimsingi ya janga hili ni umasikini. Sababu nyingine ya kimsingi ni kwamba, maarifa ya kisasa kuhusu jinsi ya kulinda afya na ukuaji mzuri wa watoto, hayajawafikia watu wengi. Kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha kinasaidia kueneza elimu hii. Lakini, uzoefu umeonyesha kwamba, kutoa habari mpya kwa kurudia mara kwa mara kwa muda mrefu kutoka pande nyingi zinazoaminika ndiko kunakoweza kufanikisha elimu ya afya kuzifikia familia na jamii zote. Kitabu cha Ukweli Kuhusu Maisha kinatolewa kama changamoto ya mawasiliano ya muda mrefu kwa: - wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa - mifumo ya elimu na taaluma ya ualimu - taaluma ya uganga na huduma za afya - wataalamu wa mawasiliano katika televisheni, radio, magazeti na majarida. - viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali - waajiri na wafanya biashara - viongozi wa vyama vya wafanyakazi na ushirika - wafanyakazi wa afya ya jamii, wauguzi na wakunga - wafanyakazi wa maendeleo na mashirika ya kujitolea - vikundi vya wanawake - vikundi vya vijana - vikundi vya maendeleo katika jamii na viongozi wa kijadi - idara zote za serikali kuu na za mitaa - wasanii, waandishi, vikundi vya utamaduni na sanaa zamaonyesho na wanamichezo. Kwa ujumla , Ukweli Kuhusu Maisha ni kwa wale wote wanaoweza kutoa changamoto kubwa ya mawasiliano itakayoziwezesha familia kutumia maarifa ya kisasa katika kuwalinda watoto wa leo na wa ulimwengu wa kesho.
...
Thank you to World Health Organization
Not part of any reading lists yet
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Or check out these books being discussed
Books being discussed
Related books: Browse all