Publisher Kenya Litho, Oxford University Press
Utenzi huu unasimulia habari za Vita Vikuu vya Pili-1939 mpaka 1945. Kwa utungo fasaha, Shaaban Robert, yule mshairi mashuhuri wa Afrika ya Mashariki, anaeleza kwa nini vita hivi vilipiganwa na viliendeshwa namna gani na pande zote mbili. Karibu kila kitu muhimu cha vita hivi kinaelezwa katika utenzi huu. Hotuba muhirnu zilizotolewa na viongozi mbalimbali, na hata simu walizopelekeana, zote zimo. Mashairi yenyewe yametungwa kwa lugha nyepesi.
...