Publisher Mpango wa Dharura wa wa Rais wa Marekani wa Kukabliana na UKIMWI (PEFPAR)
Kusudi la chati hii ni kuwapa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ambao wanapokea dawa za kudhibiti virusi vya ukimwi (ARV) maelezo kuhusu ufuatiliaji wa wingi wa virusi—ikijumuisha maana ya matokeo ya kipimo cha wingi wa virusi na madhara ya kuwaambukiza watoto wao wachanga—pamoja na ushauri kuhusu tathmini ya uzingatiaji na ushauri, hasa kwa watu walio na
ongezeko la wingi wa virusi, ambao wanahitaji kupokea ushauri wa uzingatiaji ulioboreshwa. Chati hii iliundwa ili itumike na watoa huduma mbalimbali za afya (k.m. washauri wa uzingatiaji, madaktari, wauguzi, wanafamasia, wahudumu wa afya kwa jamii) ambao huwahudumia wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ambao wanaishi na HIV, pamoja na familia zao.
...