Publisher WHO - Shirika la Afya Duniani
Kutoka Shirika la Afya Duniani
Kazi ya kupanga uzazi imeendelea kubaki bila kukamilika. Mbali na maendeleo
makubwa katika miongo kadhaa iliyopita, zaidi ya wanawake milioni 120 duniani
kote wanataka kuzuia kupata mimba, lakini wao na wenza wao hawatumii njia za
kuzuia mimba. Sababu za kutotimiza mahitaji hayo ni nyingi: Huduma na usambazaji
wa njia za uzazi wa mpango haujafanyika kwa kila mahali au kumekuwa na fursa
ndogo ya uchaguzi. Woga wa kutokubaliwa na jamii au upinzani wa wenza wao
umewasababishia vikwazo vya vitisho. Woga wa athari mbaya na matatizo ya kiafya
huwafanya baadhi ya watu wasite; wengine hawana maarifa juu ya njia ya kuzuia
mimba na jinsi ya kutumia. Watu hawa kwa sasa wanahitaji kupatiwa msaada.
Zaidi ya mamilioni ya watu hutumia mpango wa uzazi ili kuepuka mimba lakini
hushindwa, kutokana na sababu mbalimbali. Wanaweza kuwa hawakupata maelekezo
yaliyo wazi juu ya namna ya kutumia mbinu hii kwa usahihi, hawakuweza kufanya
mbinu hii iwafae, hawakujiandaa vizuri kwa ajili ya madhara, au iwapo bidhaa zikiisha.
Watu hawa wanahitaji msaada bora sasa.
...