View this book in English My Hero is You
Sign up for news and free books by email!
Shujaa Wangu ni Wewe
Jinsi watoto wanavyoweza kupambana na COVID-19
Publisher IASC - Inter Agency Standing Committee
Published 2020
sw
Pages 22
Hadithi na sanamu kuhusu jinsi watoto wanavyoweza kupambana na COVID-19. Kitabu hiki ni mradi uliotengenezwa na Kikundi cha Rufaa cha Kamati ya Kudumu ya Asasi Mbalimbali juu ya Afya ya Akili na Msaada wa Kisaikolojia katika Mazingira ya Dharura (IASC MHPSS RG). Mradi umesaidiwa na wataalamu katika ngazi za kidunia, kikanda na kitaifa kutoka Asasi Wanachama wa IASC MHPSS RG, pamoja na wazazi, walezi, walimu na watoto kwenye nchi 104. Utafiti wa kimataifa ulitolewa kwa kiarabu, kiingereza, kiitaliano, kifaransa na kihispania kutathmini mahitaji ya afya ya akili na ya kisaikolojia kwa watoto wakati wa mlipuko wa COVID-19. Mpangilio wa mada za kuelezewa kupitia hadithi hii ulitengenezwa kupitia matokeo ya utafiti. Kitabu kilisambazwa kupitia masimulizi kwa watoto katika nchi mbalimbali zilizoathirika na COVID-19. Maoni kutoka kwa watoto, wazazi na walezi yalitumika kuboresha hadithi hii. Zaidi ya watoto, wazazi, walezi na walimu 1,700 kutoka sehemu mbalimbali duniani walichukua muda wao kutuelezea kwa njia gani wanakabiliana na janga la COVID-19. Shukrani zetu za dhati kwa hawa watoto, wazazi wao, walezi na walimu kwa kushiriki katika utafiti wetu na kuwezesha hadithi hii. Hii ni hadithi iliyotengenezwa na watoto na kwa watoto ulimweguni kote.
...
see also: 555 My Hero is You translation: 555
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.