Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Mmeza fupa
Kimeandikwa na Ali Hilal Ali Hilal Ali
Mchapishaji Mkuki na Nyota
Mwaka 2019
sw
Kurasa 212
Riwaya ya Mmeza Fupa ni riwaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017. Katika tangazo la ushindi wa riwaya hii, jopo la majaji lilitoa sifa zifuatazo: Si mno mtu kukutana na riwaya ya Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, na bila ya kuonesha dalili zozote kwamba imelazimishwa. Wahusika wake wote wamebuniwa kwa ustadi, na kupewa kazi mwafaka za kuziwakilisha tanzu na matabaka mbalimbali ya jamii – pamoja na mikinzano na mazingira yao ya kihistoria, kisiasa, kisaikolojia, kitamaduni, kimjini au ya kijijini. Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni, masuala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale masuala sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi. Riwaya hii inatudhihirishia mandhari mapya ya utanzu huu wa fasihi ya Kiswahili. Uzito wa mivutano ya karne na migongano ya zama hubebwa migongoni mwa mwanadamu. Huchuana na wakati, katika kupapatuana na tsunami ya matendo ya mwanadamu. Ndivyo alivyoibuka Bi. Msiri kwenye joto la visasi, akaponea chupuchupu kumezwa na chatu-binadamu. Siku ya kuteketezwa kwa familia yake yeye alikuwa mtoni kufua. Aliporudi nyumbani alipokewa na simanzi nzito na rekecho la harufu ya damu. Hapo hapakumweka, huo ukawa mwanzo wa yeye kuwa mfungwa huru, akalimeza fupa ndani ya mapito ya karne mbili zilizompitia utosini. Kwa kuwa kwake mgubia chumvi nyingi chini ya jua, aliyajua mengi yaliyotiwa kapuni wakati ule. Akaweza kuja kuyasimulia wakati mwengine kwa vijana wengine aliowaamini. Kuhusu Mwandishi Ali Hilal Ali ni mwandishi chipukizi aliyeibuka mitandaoni kwenye uandishi na hatimaye kuingia vitabuni. Ni mzaliwa wa Kisiwani Pemba, Zanzibar. Ni mwandishi anaeogelea bahari zote – Riwaya, hadithi fupi, ushairi na tamthilia. Miongoni mwa kazi zake zilizochapishwa ni Riwaya ya Safari yangu na Diwani ya Kurasa Mpya (Fungamano la Malenga).
...
link: https://mkukinanyota.com/product/mmeza-fupa/
...
ISBN: 998708379X
Shukrani kwa Mkuki na Nyota
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Create an account to...
View comments and discuss this book!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.