You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Machozi Yamenishiya
Publisher Mkuki Na Nyota Publishers
Published 2019
sw
Pages 104
Mateso, maumivu na siasa ni mambo yaliyojaa uchochezi mkali unaomsukuma mshairi kuzungumza waziwazi na kinagaubaga na hatimaye kumfanya mwandishi apandwe na jazba zinazofanya kazi fulani itoke nje ya kingo za ulingo wa kisanaa. Katika hali kama hii, mshairi lazima atunge wimbo unaoimbika ndani ya nafsi yake mwenyewe kwanza, wimbo utakaomwezesha kunyanyuka kitandani asubuhi huku akijua hayuko pweke, ana wenzake wenye maumivu kama au kuliko yake. Mohammed Khelef Ghassani ana weledi huu wa kubaki ndani ya kingo za ulingo wa kisanaa, weledi wa kuichenga siasa kwa namna ya kuipa nguvu kubwa zinazoficha na kuzimua unagaubaga na hata ukali wake. Kuhusu Mwandishi Mohammed Khelef Ghassani alizaliwa mwaka 1977 visiwani Zanzibar na ni mwandishi wa diwani kadhaa za ushairi, zikiwemo Andamo: Msafiri Safarini Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea na N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini, ambayo ndiyo iliyompatia tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Mabati-Cornell mwaka 2015. Mbali na kuwa mshairi, Mohammed Ghassani ni mwandishi wa habari anayeishi na kufanya kazi zake nchini Ujerumani.
...
link: https://mkukinanyota.com/product/machozi-yamenishiya/
...
ISBN: 9987083757
Thank you to Mkuki Na Nyota Publishers
1 copy
Available for free in Arusha! Request