Tiba Ya Ugonjwa Wa Mawazo
Kimeandikwa na S. L. Makonga
Mchapishaji Mkuki na Nyota
Mwaka 2015
sw
Kurasa 93
Mawazo yana nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu,yanaweza kumjenga vyema mtu au kumharibia maisha yake yote. Mara nyingi tunajiwekea mawazo vichwani mwetu ambayo hutufanya tujione wadhaifu na duni, lakini mawazo hayohayo sio sahihi na kama tu tukipata tiba iliyotabibu twaweza kuyashinda mawazo hayo potofu. Tiba ya Ugojwa a Mawazo ni kitabu kitakacho kufunza juu yamawazo potofu na kakuonesha athari zake, lakini pia kukupa suluhu/tiba ya mawazo haya yasiyojenga na yanayoweza sababisha madhara makubwa katika maisha yetu. Katika jamii zetu wapo watu wengi sana ambao kwasababu fulani wamekua wakijiona wadhaifu na kudhani watu fulani ni bora na wanaweza zaidi yao. Si kweli! Kila mtu ana uwezo mkubwa wa kuwa atakavyo na uwezo huu mkubwa na waajabu upo katika mawazo ya kila mwanadamu; mawaze yako yakiwa chanya na matokeo yake huwa chanya na vivyo hivyo mawazo yakiwa hasi matokeo yake ni hasi. Kwa makusudi kabisa mwandishi amezitumia methali tuzitumiazo kila siku kama vichwa vya insha ili kuonesha jinsi methali hizo zinavyohusiana na mawazo yetu na zinavyoweza kuwa chachu ya tiba ya mawazo potofu. Kusudio la kitabu hiki ni kuwasaida watu wa rika mbalimbali na jinsia zote, wasomi na wasio wasomi, jinsi ya kuitumia guvu ya ajabu iliyo katika mawazo kusababisha matokeo mazuri na ya ajabu katika maisha yetu. Hivyo yeyote atakaye amua kuzingatia ushauri na mafundisho haya muhimu katika kitabu hiki, ndiye tu ayeweza kunufaika.
...
ISBN: 9987082998
Shukrani kwa Mkuki na Nyota
nakala 1
Kinapatikana Arusha bila malipo! Omba
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.