Publisher Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mitaa zinahitaji kuwa na usimamizi wa fedha ulio madhubuti na kiwango cha juu cha uwajibikaji kwa wananchi kuhusu Matumizi ya fedha za ruzuku zinazopokelewa kutoka Serikalini pamoja na fedha zihazokusanywa na Vijijl na Mitaa.
Mwongozo huu unatoiewa ili kuongeza udhibiti na uwajibikaji katika kusimamia fedha ngazi ya Kijiji na Mlaa. Mwongozo utasadia katika:
• Kuandaa na kusimamia bajeti.
• Kuboresha utunzaji wa vitabu vya uhasibu katika serikali za VTjiji na Kamafi za Mitaa.
• Kuweka kumbukumbu muhimu za kihasibu kwa kuzingatia kanuni za uhasibu.
• Kuwa na mfumo wa aina moja ya utunzaji vitabu katika ngazi ya Kijiji na Mtaa.
• Kuelezea jinsi ya kuandika taarifa mbalimbali za fedha.
• Kuwezesha utoaji wa taarifa katika mfumo unaowezesha Serikali na Halmashauri za Miji na Wilaya na wadau wengine kupata picha halisi ya ufanisi, na Kufanya ulinganisho wa utendaji baina ya Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mitaa.
Licha ya kuwasaidia Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata kumudu majukumu yao ya kuisimamia masuala yanayohusu fedha. Mwongozo huu una umuhimu katika nyanja nyingi ikdwa ni pamoja na:
• Kuhakikisha Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mitaa zinaweka na kutunza kumbukumbu za fedha, hali ambayo itajenga imani ya wadau katika usimamizi wa fedha za umma katika ngazi hii muhimu.
• Kuweka mfumo madhubuti wa udhibiti wa ndani, kulinda usala wa mali na rasilimali zote za Vijiji na Mitaa.
• Kuwezesha Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa kupata taarifa sahihi na muhimu zinazosaidia katika kutengeneza mipango, kudhibiti shughuli na kusaidia kutoa maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.
• Kuelekeza kwa njia ya kuwashirikisha wadau katika Kufanya maamuzi na utekelezaji wa shughuli zao wenyewe na kujenga ari ya kufanikisha shughuli hizo, kwa kutumia taarifa sahihi za mapato na Matumizi ya fedha.
Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Serikali za Mltaa, pamoja na kanuni na viwango vya uhasibu vilivyoidhinishwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
Maelezo katika Mwongozo huu yanatolewa kwa Lugha nyepesi na ya kawaida, ili kuwawezesha watumiaji wasio na uelewa wa utunzaji vitabu vya Hesabu kuelewa, kuufuatilia na kutekeleza.
Mwongozo huu wa Usimamlzi wa Fedha katika ngazi ya Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa umetokana na sera ya Serikali ya kutoa madaraka kwa kukobidhi kazi, haki. Wajibu pamoja na rasilimali fedha kwa wananchi kupitia Serikali za Mitaa. Aidha, ongezeko la fedha zinazoenda moja kwa moja vijijini kupitia mifuko ya programu mbalimbali kama Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na mashirikia yasiyo ya kiserikali, limetoa msukumo kuhusu haja ya kuwa na mwongozo huu.
...