We sponsored the creation of 3 pickleball courts in Arusha, Tanzania
Donate Play pickleball Learn more
We also sponsor monthly tennis tournaments Learn more
You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

View this book in English Vegetable Cookbook
Sign up for news and free books by email!
Kitabu cha mapishi ya mbogamboga
Kwa wanawake wajawazito na watoto
Publisher Tanzania Smallholder Horticulture Empowerment and Promotion (TANSHEP), Japan International Cooperation Agency (JICA)
Published 2022
sw
Pages 24
Download 5.0 MB
Kula mbogamboga kwa afya yako! Mradi wa TANSHEP huwawezesha wakulima kuongeza kipato zaidi kwa kuwahamisha wakulima wajue mahitaji ya soko kwanza. Unahamasisha wakulima kufanya utafiti wa masoko kabla ya kuanza uzalishaji ili kufahamu ni aina gani ya mbogamboga inahitajika, inahitajika wapi na kwa kiwango gani. Pamoja na kupanua fursa za masoko kwa ajili ya wakulima wa TANSHEP, kwanini ni mhimu sana kula zaidi mbogamboga? Kwa Tanzania, upungufu wa virutubisho na utapiamlo vimekua ni tatizo kubwa la kudumu. Upungufu wa viini lishe ni moja ya sababu kuu ya kudumaa miongoni mwa watoto, na utapiamlo unaweza kusababisha si tu magonjwa yasiyo ambukiza kwa ujumla lakini pia unaweza kuwaweka akina mama wajawazito katika hatari. Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ulaji wa mboga za majani Tanzania upo kwa kiwango cha chini sana ya kiwango cha kidunia kilichopendekezwa na WHO. Kwa kuamini kwamba ufahamu wa walaji juu ya matokeo chanya ya ulaji wa mboga za majani na kubadilika katika tabia za ulaji itapelekea kukua kwa soko la mbogamboga na kuimarisha hali ya lishe Tanzania kwa mda mrefu. TANSHEP ilianza majukumu ya kuhamasisha shughuli ya kuinua uelewa wa ulaji wa mbogamboga kwa walaji wa Kitanzania hasa kwa wanawake wajawazito na watoto. Katika kazi za hivi karibuni, TANSHEP imetengeneza mapishi ya mbogamboga kwa kushirikiana na maafisa wa wilaya kutoka sekta za kilimo na afya ili kuimarisha hali ya lishe kwa watoto na akina mama. Mapishi yote yanatumia virutubisho vyenye wingi wa mbogamboga ambazo wakulima wa TANSHEP wanazalisha au wanaweza kuzalisha hapo baadae. Kupitia mapishi na matukio ya maonesho (kwa vitendo) ya upishi, washiriki wanatarajia kujifunza lishe muhimu kwa ajili yao wenyewe na watoto wao, namna sahihi ya kupika mboga za majani kwa namna ya kutopoteza virutubisho na kujaribu kupika mboga za majani kwaajili ya matumizi ya nyumbani.
...
TANSHEP (mradi wa uwezeshaji na uhamasishaji wa kilimo cha mbogamboga kwa wakulima wadogo Tanzania) ni mradi unaojikita katika kutatua changamoto ya masoko ya mazao ya mbogamboga, unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo na TAMISEMI kwa ufadhiri wa shirika la maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga.
...
Thank you to Tanzania Smallholder Horticulture Empowerment and Promotion (TANSHEP), Japan International Cooperation Agency (JICA)
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all