You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Fungua akaunti mpya

Taarifa
Majadiliano
Methali
Usilolijua ni kama usiku wa giza
ili kupiga kura
Kura
14
"na Ibrahim Nyanda
🏆 Shindano la Insha ya Methali
“Ni kwa nini kijiji chetu hakina maendeleo ukilinganisha na vijiji vingine vinavyotuzunguka? Vijana wengi kutoka vijiji vingine wa umri wetu wamesoma na wengine wana kazi zao za maana huko mjini. Pamoja na kwamba kuna shule kijijini kwetu lakini vijana hatufanyi vizuri shuleni na hata walimu wanapoajiriwa hawakai muda mrefu wanahama. Kuna nini hapa Bombambili?" Haya ni maswali ambayo kijana Akilimali alimwuliza rafiki yake Manase wakiwa machungani wakilisha ng’ombe. 

Mara baada ya swali hili Manase alionekana amezama katika wimbi kubwa la mawazo na mara baada ya kufikiri kwa muda alimgeukia rafiki yake Akilimali na kumtazama kwa kina kiaha akamwuliza, “Unaamini kuhusu ushirikina” Akilimali alijibu kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na swali aliloulizwa na kisha akasema “Naamini kwani mara kadhaa nimekua nikiona watu wakienda kwa waganga na wengine wanapopitia magumu huamini wamerogwa, si unakumbuka juzi bibi Andunje tulivyoambiwa kuwa amekutwa juu ya paa la mzee Masanja uchi wa mnyama akiwanga, sasa mpaka hapo naachaje kuamini mshikaji wangu” 

Manase alimwangalia Akilimali kwa makini kisha akamwambia, "Nataka nikueleze siri moja ambayo huwezi amini……. hivi unajua kama mama yako na dada yako ni wachawi?” Akilimali alibaki ameduwaa mithili ya mjusi aloyebanwa na mlango halafu akiwa amefura kwa hasira akamwambia Manase “Aisee mwanangu usianze kuniletea habari zako za udwanzi hapa, tena koma kabisa kumwambia mama yangu mchawi vinginevyo ntakuja kukufanyia kitu mbaya hutokuja kuamini macho yako, ohoooo!!” 

Manase alimtuliza rafiki ake Akilimali halafu akamwambia, “Ngoja niwarudishe ng’ombe jirani afu nikupe mchapo mzima ulivyo, najua utanielewa we punguza jaziba kwanza” 

Mara baada ya kurudisha mifugo jirani Manase akaanza kumweleza Akilimali, “Rafiki angu nataka nikupe siri hii ambayo nimekaa nayo kwa muda mrefu, chochote unachokiona hapa hata kutokuwepo kwa naendeleo kijijini ni kwa sababu ya ushirikina, kila siku mama yako na dada yako huwa ninawaona wakija nyumbani wamepanda fisi wakimpitia mama kwenda kuwanga…..” Manase alitulia kidogo halafu akaendelea 

“Huwezi kuamini kwani hata mimj nilikua siamini mpaka nilipopakwa dawa na kuwaona, nitakupa hiyo dawa utapaka machoni na utakuja kunipa majibu kesho.” 

Mara baada ya mlo wa usiku Akilimali alikua ameketi akiota moto nje ya nyumba yao ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi wakati huo mama yake na dada yake wakiwa ndani na yeye akiwa na baba yake pale nje. Alipaka ile dawa kama alivyoelekezwa na baada ya dakika kumi alimwona dada yake na mama yake wamepanda juu ya fisi mithili ya pikipiki tayari kwa safari ya kwenda kuwanga. 

“Nisamehe sana rafiki angu, ilikua ni hasira tu” aliongea maneno haya Akilimali huku akilengwa na machozi, 

“Mimi nilijua, sasa unavyoona kijijj chetu hakiendelei hata mama yako pia na dada yako wanahusika, inaumiza sana kila mwanakijiji anayetaka kuleta maendeleo anaishia kufa, lazima kuna siku watakuja kuumbuka kama ilivyokua kwa bibi Andunje” 

“Nina uhakika hata baba yako hajui kama mama yako na dada yako ni wachawi na kila siku huwa wanaenda kuwanga na ninyi kuwaachia mauzauza mkijua wapo, nenda kampake baba yako hiyo dawa alafu utanipa majibu” alieleza Manase 

Jioni kwa siri Akilimali alimweleza baba yake kuwa dada yake na mama yake ni wachawi kitu ambacho alipinga vikali. 

“Mama leo baba anatuona, angalia anvyotutumbulia macho” dada yake na Akilimali alimwabia mama yake wakiwa juu ya fisi kama ilivyo ada wakati baba yake na kaka yake wakiwa nje wanaota moto kama ilivyo kawaida yao. 

“Sidhani kama anatuona, hebu geuza fisi tuwe kama tunawaelekea wao” ailisema mana yake na Akilimali.

Akilimali anasema hiyo ndiyo ilikua siku ya mwisho kumwona baba yake kwani baada ya kuona fisi aliyewabeba mke wake na binti yake alitimua mbio kama anashundana mashindano ya mbio za mita mia. Ama kweli usilolijua ni kama usiku wa giza, Akilimali alibaki haamini kama kwa muda wote huo ameishi na mama yake na dada yake bila kujua kuwa ni wachawi. 
Marejeleo

Chimbuko:

Methali ya kiswahili kutoka kitabu cha “METHALI ZETU” cha Oxford inayosema “USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA.”  

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishika nafasi ya nne katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Ibrahim Methusela Nyanda ni Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Ibrahim Nyanda
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org
Loading...
Loading...
Ingia akaunti yako ili kuona na kutoa maoni

Ufafanuzi


Methali hii ya Kiingereza inatafsirika pia kama "Kalamu ina nguvu kuliko upanga au jambia" au " Kalamu ni kali kuliko upanga." Katika methali hii, jambia au upanga unaashiria nguvu na ukatili, na maana ya kalamu ni maneno. Ingawa upanga unaweza kushinda kwa nguvu, kalamu inaweza kuwashawishi, kuwahamasisha, na kuwaelimisha watu. Sio kila mtu ana silaha za kuwalazimisha watu wengine kufanya kile anachotaka, lakini kila mtu ana uwezo wa kubadilisha ulimwengu kupitia kile anachofikiria, kusema na kuandika kwa maneno. 

Silaha za siku hizi ni kalamu na karatasi.
 - Methali ya Kiswahili

Methali hii ni kweli kwa sababu mara nyingi maneno huchochea na kudhibiti jinsi watu wanavyotumia nguvu na silaha zao. Kwa mfano, kupitia sheria, maneno ya viongozi, mahakimu na majaji yana uwezo wa kuwafunga watu gerezani au hata kuwaua. Kutoa hotuba ya moto kwa umati wa watu wenye hasira kunaweza kuleta ghasia kali na madhara mengine (ona Juliasi Kaizari).

"Ukinipa picha, nitakupa vita."
- William Randolph Hearst
(Mwandishi wa habari na mchapishaji wa magazeti, Marekani)

Lakini pia, methali hiyo inatukumbusha nguvu ya upinzani usio na vurugu kwenye kuleta mabadiliko ya kudumu, kanuni iliyotetewa na kuonyeshwa na watu kama Mahatma Gandhi, Martin Luther King, na Nelson Mandela.  Angalia pia: Insha ya "Civil Disobedience"  na Henry David Thoreau, pamoja na Tamthilia mashuhuri ya "Antigone" na Sophocles.

Chimbuko


Nukuu hii ya "kalamu ina nguvu kuliko upanga" ilipata umaarufu kupitia tamthilia ya "Richelieu: au The Conspiracy"  na Edward Bulwer-Lytton (mwaka wa 1839, ukurasa wa 47). Lakini hakika wazo lilikuwepo kabla.

Wengine wanasema chimbuko halisi la methali hii ni Hadithi ya Ahikar. Kitabu hiki kiliandikwa takriban miaka 600 kabla ya kristu, na ni chimbuko la methali zingine kama "Ndege mkononi ana thamani ya wawili mtini"). Katika toleo letu, mfasiri hakuweza kusoma maandishi kutokana na hali ya karatasi, na maneno yalikatika. (Ukurasa 171/274) 
Dhibiti kinywa chako kwa uangalifu ...[ILIKATA]... na ufanye moyo wako kuwa mzito(?), kwa maana neno linalosemwa ni kama ndege, naye alitamkaye ni kama mtu asiye na  ...[ILIKATA]... ufundi wa maneno una nguvu zaidi kuliko ufundi wa  ...[ILIKATA]...
- Hadithi ya Ahikar, Ukurasa wa 171/274
Je, hili ndilo chimbuko halisi la methali hii, miaka zaidi ya 2,500 iliyopita? Muwe majaji...

Chanzo karibu na methali hii pia kinaonekana katika Agano la Kale:
Kwa maana neno la Mungu ni hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili.
Waebrania 4:12, Biblia

Na vilevile katika Shakespeare: 
Wengi wanaovaa panga huogopa kalamu.
-William Shakespeare
Tamthilia ya Hamlet, Sehemu ya 2, Onyesho la II (ukurasa wa 59)

 Je, unakubali kalamu hushinda jambia? Toa maoni yako hapo chini!
...

CC BY Unaruhusiwa kunakili & kusambaza mchoro huu na makala hii bila idhini, ukitaja tu chanzo (www.maktaba.org)

Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Watu wengi wanaogopa kuuliza maswali kwa sababu wanahofia kuonwa mjinga. Lakini kuuliza maswali ni njia bora ya kujifunza kutoka kwa wengine. 

Pia kuuliza maswali husaidia wenzako. Je umewahi kusita kuuliza swali kwani ulidhani wengine wameshaelewa... lakini baadaye uligundua hawakuelewa pia? 

Kiingereza
There's no such thing as a stupid question
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
That which draws our attention, gets more attention. 

A wheel that makes noise is more likely to receive oil than other wheels (that also might need oil). We have limited attention, and thus we give our attention to people, projects and problems that stand out. This proverb asserts that there is not necessarily a correlation between the things we give our attention to and the things that actually need our attention.

Another version of the proverb is "the squeaky wheel gets the grease," and though the origin is unknown, American humorist Josh Billings is commonly attributed through his poem "The Kicker" in 1870
I hate to be a kicker,

I always long for peace,

But the wheel that squeaks the loudest,

Is the one that gets the grease.
 
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
As the appetite increases, food tastes better.

The proverb first appeared in Miguel de Cervantes' Don Quixote, published in 1615 (in Part II, Chapter V)

Parents often say this to their children when they are fussy eaters.
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by