na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿 🏆 Shindano la Insha ya Methali 🥉 Mshindi wa Tatu
Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho linatiririka
Jua limezama Sasa kasia ufukweni, hoi kitandani, nyavu zi baharini
Nyumbani mtaa wa nne, nahodha wa familia surubu nivute kheri
Jua Sasa la chomoza, Kiguu na njia kulitafuta tonge
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Creative Commons Attribution (CC BY 4.0) na Magreth Lazaro Mafie Ilichapishwa na Maktaba.org Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org
[M]tu hawezi kupata uzoefu wa mambo yote yahusuyo maisha kutoka kwa wazazi wake: lazima awe tayari kufunzwa na ulimwengu, yaani kujifunza kutoka kwa wengine zaidi ya baba na mama yake.
Silaha za siku hizi ni kalamu na karatasi.
- Methali ya Kiswahili
"Ukinipa picha, nitakupa vita."
- William Randolph Hearst
(Mwandishi wa habari na mchapishaji wa magazeti, Marekani)
Dhibiti kinywa chako kwa uangalifu ...[ILIKATA]... na ufanye moyo wako kuwa mzito(?), kwa maana neno linalosemwa ni kama ndege, naye alitamkaye ni kama mtu asiye na ...[ILIKATA]... ufundi wa maneno una nguvu zaidi kuliko ufundi wa ...[ILIKATA]...
- Hadithi ya Ahikar, Ukurasa wa 171/274
Kwa maana neno la Mungu ni hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili.
Waebrania 4:12, Biblia
Wengi wanaovaa panga huogopa kalamu.
-William Shakespeare
Tamthilia ya Hamlet, Sehemu ya 2, Onyesho la II (ukurasa wa 59)
CC BY Unaruhusiwa kunakili & kusambaza mchoro huu na makala hii bila idhini, ukitaja tu chanzo (www.maktaba.org)
Unaweza kusafiri kwa meli peke yako,
kulala au kupumzika peke yako.
Unaweza kuingia kwenye deni peke yako.
Kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya peke yako.
Lakini ni lazima muwe wawili ili kucheza tango, muwe wawili ili kucheza tango...
ايد لوحدها ماتسقفش
Mkono mmoja hauwezi kupiga makofi
Bila mtu wa pili ugomvi hauanzi
Kidole kimoja hakiuwi chawa
by Nankya Sauda 🇺🇬 🏆 Proverb Essay Contest 🥇 First Place Winner
“The monotony and solitude of a quiet life stimulates the creative mind.”
“Smooth runs the water where the brook is deep”