Leo tuna furaha kubwa kutangaza washindi wa Shindano la kwanza la Insha za Methali la Maktaba.org. Kwanza kabisa tunataka kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote walioshikiri katika shindano hili. Mmetufundisha vingi, asanteni!

➡️ Insha zote ⬅️


🏆 Tangazo la Washindi

Sasa bila kupoteza muda, tuwapongeze Washindi wa Shindano la kwanza la Insha ya Methali:

🥇 Mshindi wa nafasi ya kwanza:
Nankya Sauda 🇺🇬 Uganda
kwa insha yake juu ya methali
➜“Still waters run deep

🥈 Mshindi wa nafasi ya pili:
Rose Mwanri 🇹🇿 Tanzania
kwa insha yake juu ya methali
➜“Akiba haiozi

🥉 Mshindi wa nafasi ya tatu:
Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿 Tanzania
kwa insha yake juu ya methali
➜“Mchumia juani hulia kivulini

Pongezi kwa wote walioshiriki!

   Washindi hawa watatu wameshapokea zawadi zao, na wandishi wote walipewa vyeti vya kutambua michango yao. (Kama haujapokea cheti chako, tafadhali wasiliana nasi.)
   Shindano hili lilifanyika kwajili ya Siku ya Kiswahili Duniani (Maadhimisho ya Siku ya Saba Saba). Hili ndilo shindano la kwanza tulilofadhili mtandaoni. Tunaomba shauri zenu, toeni maoni hapo chini, lifanyike tena? Kutokana na mwitikio mkubwa wa watu katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, tayari tunaanza kupanga.
   Kama ulikosa kuwashilisha insha yako, usikose kushiriki shindano lijalo. Jiunge nasi, thibitisha email yako na utajulishwa.