Tunaomba msaada wako! 

Je unapenda kuandika? Unapenda Methali ya Siku? Maktaba.org tunasherehekea Siku ya Kiswahili Duniani kwa Shindano la Uandishaji wa Insha!

Wasilisha Insha ya Methali kabla ya 7/7

Wasilisha insha yako juu ya methali yoyote hapa au kwa baruapepe tuzo@maktaba.org leo ujipatie nafasi ya kushinda zawadi ya pesa!
  1. Mshindi wa kwanza 50,000/= TSh
  2. Mshindi wa pili25,000/= TSh
  3. Mshindi wa pili12,500/= TShl

Vigezo & Masharti ya Shindano

Washindi watachaguliwa na watumiaji wa Maktaba.org! Insha tatu zitakayopata "likes" ❤️ nyingi zaidi kabla ya trh 15 July watashinda. Mtu yeyeote anaweza kupiga kura akiingia akaunti ya yake ya Maktaba.org (Kama haujafunguliwa akaunti yako, jiunge leo, bila malipo yoyote!) 

Hatua ya 1: Chagua methali. Methali inaweza kuwa kwa lugha yoyote, lakini sharti iwe methali inayojulikana na watu, yaani usitunge mwenyewe. Unaweza kutafuta katika vitabu vyetu vya methali hapa!

Hatua ya 2: Tunga insha inayoeleza maana ya methali kwa maoni yako.

Masharti (lazima)
  1. Lugha: Insha iwe kwa Kiswahili ama kwa Kiingereza.
  2. Urefu: Idadi ya maneno ya insha iwe kati ya 80 na 1000 (ndefu kuliko aya, ila isizidi kurasa. Piga chapa kwa kompyuta au simu.
  3. Hakimiliki: Insha yako itasambazwa chini ya leseni ya Creative Commons (CC BY 4.0), inayosema, kwa kifupi, inaruhusiwa kunakili, kubadilisha, kutafsiri na kuchapisha kazi yako bila idhini, kama utatajwa kama mtungaji.  

Ushauri (hiari)
Haya ni mawazo kwa muundo wa insha yako:
  • Chimbuko: Eleza chimbuko la methali kama inajulikana. Taja vyanzo vya taarifa.
  • Matumizi na mifano: Methali hutumika vipi na nyakati gani? Taja mifano.
  • Bunilizi: Tunga shairi au simulia hadithi fupi iniayohusiana na maana ya methali.
  • Uzoefu binafsi: Simulia hadithi kutoka kwa maisha yako / uzoefu wako mwenyewe.
  • Utekelezaji: Toa shauri kwa wasomaji jinsi ya kutekeleza methali katika maisha yao ya kila siku.
  • Simulizi ya kweli: Shiriki hadithi kutoka sayansi, historia, ngano/kisa, dini, au fashihi. Taja vyanzo halisi.
  • Methali zinazohusiana: Find similar proverbs from around the world.
  • Methali zinazopingana: Je kuna methali ambazo zinatofautiana na methali hii?
  • Majadiliano: Uliza maswali yanayowaalika wasomaji kutafakari na kushiriki mawazo yao / uzoefu wao.
  • Picha/Mchoro: Chora, piga, au tafuta picha inayoeleza maana ya methali na ambatanisha katika insha yako.
Hayo ni mawazo tu, ili kukuhamasisha. Pia unaweza kusoma mifano kwenye Methali za Siku. Tunatarajia kuona ubunifu wako!

Hatua ya 3 : Pakia (upload) insha yako hapa
Tarehe ya mwisho: 7 Julai 2023 (Saba Saba)
Jaza fomu: https://forms.gle/2VgUtNPMBLETjbCx5
AMA unaweza kuwasilisha insha yako kwa baruapepe. Tuma kwa tuzo@maktaba.org. Usisahau kutuambia taarifa zako za malipo ili tuweze kukutumia zawadi ya pesa ukishinda shindano!

Wasilisha insha hapa kabla ya 7/7/23