We sponsor book clubs in Arusha, Tanzania
Read more Learn more
Posts / Proverbs Proverb of the day
SW

Haraka haraka haina baraka

Methali ya leo ni "Haraka haraka haina baraka." Tafsiri yake kwa Kiingereza ni "Haste makes waste" au "Hurry hurry has no blessing" Mnaonaje - tafsiri ipi bora? Toeni maoni chini... 

Kwa upande wangu naona kwa mitazamo miwili. Methali hii inaweza kutufundisha:
  1. Subira: Haraka husababisha makosa, na makosa hutuzuia baraka. (Nenda taratibu)
  2. Mindfulness (yaani uwepo kiakili na utulivu): Tunapopoenda kwa haraka, hakuna muda wa kutambua, kutumia au kufurahia baraka tulizo nazo. 

Kuna misemo karibu na "haraka haraka haina baraka" katika nchi nyingi. Mifano: 
Kihispania: 
No por mucho madrugar amanece más temprano
(Kuamka mapema hakufanyi jua kuchomoza mapema)
Kifaransa: 
Tout vient a point a qui sait attendre
(Everything comes to those who wait)
Kiswahili:
 Pole pole ndio mwendo 
Kichina: 
欲速则不达
Methali hii ya Kichina ni karibu na "Haraka haraka haina baraka". Inatoka kitabu cha Misemo ya Konfusio (Analects, 13:17, ona ukurasa wa 92):
Tsz-hiá alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Kü-fu, aliomba ushauri wa Konfusio juu ya serikali,  Konfusio akajibu "Usitamani matokeo ya haraka. Usiangalie faida ndogo. Ukitaka matokeo ya haraka, hayatakuwa ya mbali; na ukizingatia faida ndogo huwezi kukabiliana vizuri na mambo muhimu."

Katika kitabu cha  "Methali za Kiswahili Zaidi kutoka Afrika Mashariki" waandishi Kalugila na Lodhi walitaja methali hii kama mfano mzuri wa mtindo wa ushauri katika methali:
Kwa mujibu wa tarehe/historia, yaelekea kuwa mithali zilitangulia tungo za ushairi, na watungaji wa Kiswahili walikuwa na fursa ya kutumia hazina kubwa ya mithali zilizohifadhiwa na wakuzaji wa masimulizi na mapokeo ambao wengi wao walikuwa wanawake. Mithali za hapo mwanzoni bila shaka zilitungwa kwa mitindo ya ushairi ambayo polepole ikatakata na kuweka imara miundo ya arudhi/prozodi zilizokubaliwa kuwa za kawaida. Mithali za Kiswahili za kawaida mno, na zilizo fupi pia, ni zenye mizani 6, 8, 12 au 16. Nyingi zao hutumika katika tunga kama mistari, vipande au mikarara/vipokeo. Kuna mifano ming i ya mashairi yanayoanzia na mithali fulani na pia ni maelezo marefu ya mithali yenyewe.Katika mifano ifuatayo kutoka mashairi mbalimbali kuna ikaa (mwendo wa ulinganiful ya 3 + 3, yaani mizani 6 parnoja na kituo cha kati na mkazo kwenye mizani ya mwisho ila moja: [Mifano:] Akili ni mali. Mahaba ni haba. Mapenzi majonzi.
Kituo katika mithali na fumbo kisababishacho vipande 2, 3 au 4 ni sawa na kituo chenye ikaa/mwendo katika mashairi ya vina yenye mizani kamiIi zinazolingana. Vina vyenyewe vinaweza kuelezwa kama ifuatavyo. [Mifano]:
Haraka haraka / haina baraka (aaba, 3+3/3+3)
(Kwa) haba na haba / hujaza kibaba. (aaba, 3+3/3+3)
 
Niliuliza Akili Bandia "Nifanye nini ili kutekeleza methali ya "haraka haraka haina baraka katika maisha yangu ya kila siku?" Hapa ni shauri zake: (Nilihariri nukuu)
Kuweka Mipango: Kabla ya kuanza kazi/mradi, chukua muda wa kuweka mipango. Gawanya kazi kubwa katika hatua ndogo zinazoweza kudhibitiwa, na ujipe muda wa kutosha kukamilisha kila hatua vizuri.
Kufanya Maamuzi: Usifanye maamuzi kwa haraka na ya haraka, hasa kuhusu mambo muhimu. Orodhesha chaguzi zako zote, pima faida na hasara, tafuta ushauri, kisha ufanye chaguo sahihi.
Kujifunza: Badala ya kujaribu kusoma kitabu, darasa au zoezi la nyumbani kwa haraka, nenda polepole, jiulize maswali, soma tena na tena hadi uelewe nyenzo kikamilifu. Kwa njia hii utajifunza kweli na kukumbuka habari, badala ya kuisahau haraka. Pia utafurahia kujifunza mengi zaidi!
Mahusiano: Kujenga mahusiano imara huchukua muda. Iwe na marafiki, familia, au mapenzi, usikimbilie. Wekeza muda katika kumfahamu mtu, kumwelewa, na kujenga msingi imara.
Kazi: Zingatia ubora kuliko kasi, na uchukue muda wako wa mapumziko ili kuepuka uchovu. Epuka kuharakisha kazi zako ili kuzimaliza haraka. Ukienda haraka hautafanya kazi yenye ubora wa juu, lakini pia kufanya kazi kwa makini hukusaidia kujifunza na kukua.
Afya: Usitafute suluhisho la haraka wala njia za mkato katika masuala ya afya yako. Mazoezi, chakula safi, na mapumziko ni muhimu, na yote yanahitaji muda.
Kujiboresha: Ukuaji na maendeleo ya kibinafsi ni mchakato wa muda mrefu. Usiharakishe. Weka malengo yanayoweza kufikiwa, yafanyie kazi hatua kwa hatua, na uthamini ushindi mdogo unaoendelea.
Mindfulness (uwepo wa kiakili): Kuwa makini na mahali ulipo na kile unachokifanya. Wakati wa kula, furahia ladha kile unapotafuna. Unapozungumza na mtu, mzikilize kwa makini. "Haraka haraka haina baraka" inatufundisha maisha ni safari. 
Naona Akili Bandia alinipa ushauri mzuri wa busara... Ningependa kujua maoni yenu :)

Vitabu Vinavyohusiana:
More Swahili Proverbs from East Africa: Methali zaidi za kiswahili toka Afrika Mashariki by Leonidas Kalugila and Abdulaziz Y. Lodhi, ukurasa wa 77
Methali za Kiswahili - Swahili Proverbs ukurasa wa 202
Misemo ya Konfusio - Analects, 13:17, ukurasa wa 92 (Kiingereza kutoka Kichina)
Interpersonal Communication - A Mindful Approach to Relationships 

Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Are you traveling to Tanzania?

Learn Useful Phrases in English & Swahili

Master essential everyday phrases in both languages