Tunaomba msaada wako!
Wasilisha Insha ya Methali kabla ya 7/7
- Mshindi wa kwanza ➜ 50,000/= TSh
- Mshindi wa pili ➜ 25,000/= TSh
- Mshindi wa pili ➜ 12,500/= TShl
Vigezo & Masharti ya Shindano
- Lugha: Insha iwe kwa Kiswahili ama kwa Kiingereza.
- Urefu: Idadi ya maneno ya insha iwe kati ya 80 na 1000 (ndefu kuliko aya, ila isizidi kurasa. Piga chapa kwa kompyuta au simu.
- Hakimiliki: Insha yako itasambazwa chini ya leseni ya Creative Commons (CC BY 4.0), inayosema, kwa kifupi, inaruhusiwa kunakili, kubadilisha, kutafsiri na kuchapisha kazi yako bila idhini, kama utatajwa kama mtungaji.
- Chimbuko: Eleza chimbuko la methali kama inajulikana. Taja vyanzo vya taarifa.
- Matumizi na mifano: Methali hutumika vipi na nyakati gani? Taja mifano.
- Bunilizi: Tunga shairi au simulia hadithi fupi iniayohusiana na maana ya methali.
- Uzoefu binafsi: Simulia hadithi kutoka kwa maisha yako / uzoefu wako mwenyewe.
- Utekelezaji: Toa shauri kwa wasomaji jinsi ya kutekeleza methali katika maisha yao ya kila siku.
- Simulizi ya kweli: Shiriki hadithi kutoka sayansi, historia, ngano/kisa, dini, au fashihi. Taja vyanzo halisi.
- Methali zinazohusiana: Find similar proverbs from around the world.
- Methali zinazopingana: Je kuna methali ambazo zinatofautiana na methali hii?
- Majadiliano: Uliza maswali yanayowaalika wasomaji kutafakari na kushiriki mawazo yao / uzoefu wao.
- Picha/Mchoro: Chora, piga, au tafuta picha inayoeleza maana ya methali na ambatanisha katika insha yako.
Hatua ya 3 : Pakia (upload) insha yako hapa
Tarehe ya mwisho: 7 Julai 2023 (Saba Saba)
Jaza fomu: https://forms.gle/2VgUtNPMBLETjbCx5
AMA unaweza kuwasilisha insha yako kwa baruapepe. Tuma kwa tuzo@maktaba.org. Usisahau kutuambia taarifa zako za malipo ili tuweze kukutumia zawadi ya pesa ukishinda shindano!