Majambo ya binadamu yana kujaa na kupwa, Yakidakwa yamejaa huongoza ushindini; yakipuuzwa, safari yote ya maisha yao haiachi maji mafu, na hujaa madhilifu. Sisi sasa twaelea katika maji makuu; Twapaswa kuyatumia yangali yakitufaa, ama sivyo tutakosa yote. -Shakespeare, Juliasi Kaizari, Tafsiri ya J. K. Nyerere
There is a tide in the affairs of men Which, taken at the flood, leads on to fortune; Omitted, all the voyage of their life Is bound in shallows and in miseries. On such a full sea are we now afloat, And we must take the current when it serves, Or lose our ventures. - Shakespeare, Julius Caesar