Vitabu vya Dini
Vitabu juu ya Ukristo
Vitabu juu ya Uislamu

Kwa watu wengi, kitabu wanachokipenda zaidi ni kitabu takatifu, kama Biblia au Korani. Kwa nini tunapenda kusoma vitabu hivi kuliko vitabu vingine? 
  • - Vitabu Takatifu vinahusiana na mambo muhimu ya maisha.
  • - Vitabu Takatifu vinatupa busara na fadhili kama ujasiri, unyenyekevu, na imani.
  • - Vitabu Takatifu vina hadithi za kusisimua kuhusu manabii na mashujaa. 
Mimi nimesoma vitabu vingi takatifu kutoka dini tofauti kama vile Korani, Biblia, na vitabu takatifu vya Wahindi na Wachina. Nimetambua vina kanuni na hadithi zilezile; ni majina tu hubadilika.
Vitabu vya shule vina maswali mengi, na majibu sahihi yapo katika sehemu ya mwisho, au katika Kitabu cha Mwalimu. Ila kwa vitabu takatifu, hakuna majibu ya hakika. Wasomi na walimu wa dini bado hawakubaliani kabisa maana ya kitabu. Wanatumia elimu walionayo kujadili na wanahojiana juu ya aya muhimu. 
Kama unaamini kitabu fulani kilitoka Mungu, usimwamini mtu yeyote kukuambia kinasema nini-- Jisomee mwenyewe!
Kwa watu wengi, wakati huu ni msimu wa kutafakari dini zao, kwa sababu ya Ramadhan na Kwaresma.  Chukue nafasi hii kujielimisha kidini. 


For many people, their favorite book is a Holy Book, like the Bible or Quran. Why do we like to read these books more than others?
  • - Holy books are about the important things in life.
  • - Holy books give us wisdom, courage, humility and faith.
  • - Holy books have exciting stories about prophets and heroes. 
I've read a lot of books from different religions like Christianity, Islam, Hinduism and Confucianism. I recognized the same principles and stories-- it's just the names that change. School textbooks have many questions and the correct answers are in the last section, or in the Teacher's Book. But for Holy Books, there are no certain answers. The scholars and teachers of religion still don't completely agree on the meaning of the book. They use their education to discuss and argue about important verses.
If you believe that a certain book came from God, don't trust any person to tell you what it says-- Read it for yourself!  
For many people, this is a season to meditate on religion because of Ramadan and Lent. Take this chance to educate yourself.