View this book in English Labour and Delivery Care
Sign up for news and free books by email!
Utunzaji katika Leba na Kuzaa
Written by HEAT Health Education and Training Programme
Publisher: The Open University sw
Download 9.9 MB
This book is public domain or creative commons
Shirika la Afya Duniani (SAD) linadokeza kuwa zaidi ya watoto milioni 133 huzaliwa kila mwaka duniani kote, ambapo asilimia 90 yao huzaliwa katika mataifa yenye mapato ya wastani na ya chini. Kila mwaka, takriban watoto milioni 8 hufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 5. Idadi kubwa ya vifo hivi hutokea katika kipindi cha uzaliwani (yaani muda mfupi kabla na baada ya kuzaliwa). Kima cha vifo vinavyotokea katika uzaliwani kimekadiriwa kuwa takriban vifo milioni 7 kila mwaka (visa milioni 3.5 vya kuharibika kwa mimba na milioni 3.5 katika kipindi cha siku 7 za kwanza). Idadi hii ni zaidi ya ujumuisho wa vifo vinavyosababishwa na VVU/UKIMWI (milioni 2.1), kifua kikuu (milioni 1.6) na malaria (milioni 1.3), hali inayopelekea vifo vya watu milioni 5 kote duniani. Karibu robo ya watoto milioni 7 wanaokufa katika kipindi cha uzaliwani hutokea katika kipindi cha leba na kuzaa. Visababishi vya vifo vya kipindi cha uzaliwani na vinavyotokana na kuzaa katika mataifa yanayostawi hulingana kwa karibu (kuvuja damu, matatizo ya shinikizo la damu katika ujauzito, ekilamsia, maambukizi na leba iliyofungana). Maisha ya wanawake wengi walio katika leba na kuzaa pamoja na watoto wao yanaweza kuokolewa katika mataifa yanayostawi iwapo watahudumiwa na wakunga waliohitimu.
...
Kitabu hiki kimeandaliwa kufundisha watoa huduma na wanafunzi wa chuo. Unaweze kujiunga na kusoma bure mtandaoni Utunzaji katika Leba na Kuzaa
...
Thank you to Health Education and Training Programme (Heat) and the Open University UK
Not part of any reading lists yet
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Or check out these books being discussed
Books being discussed
Related books: Browse all