You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Stadi za Maisha Kupitia Michezo Mwongozo wa Mwalimu
Life Skills Through Games A Teacher ́s Guide
Publisher Jambo Bukoba
Published 2012
Pages 101
Download
Kitabu cha mbinu za ufundishaji na mkusanyiko wa mazoezi mbalimbali kwa ajili ya makocha na walimu wa somo la michezo. Methodology handbook and compendium of exercises for coaches and Physcial Education teachers. Mpendwa mwalimu,ukitaka kutumia michezo kama zana ya elimu kwa maendeleo na mabadiliko katika jamii ni muhimu kuwa na watu wanoweza kupanga na kuandaa shughuli za michezo zenye ubora. Unahitaji kufahamu jinsi ya kutumia vifaa na kujifunza michezo mbalimbali na sheria zake. Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuamue kuwafunza walimu wa somo la michezo katika ngazi ya chini. Wewe ni mmoja wa walimu ambao wamepata mafunzo katika warsha ya siku tano juu ya kutumia michezo ili kuboresha kujiamini kwa wanafunzi, kujenga umoja, kuboresha mawasiliano, uwajibikaji na nidhamu. Mawazo yote yanayofundishwa katika yetu kwa walimu yanajumuishwa katika kanuni hii: Michezo + Stadi Mabadiliko/Maendeleo Kanuni hii ndio inayotuongoza katika malengo ya mradi huu wa michezo. Mradi huu haulengi kuibua vipaji vipya au wanamichezo mahiri. Tunaamini kwamba michezo ni sehemu ya msingi ya elimu. Tunaamini pia kuwa afya ya mwili hujenga afya ya akili. Hivyo shughuli za mradi huu pamoja na mtaala wa warsha za walimu unaleta dhana mpya. Hatuhitaji kuona watoto wakikimbia kwa kasi zaidi, wakiruka juu zaidi au kupiga mpira golini kama kipaumbele. Tunataka kuchangia katika mabadiliko ya jamii, tunataka kusaidia kuleta maendeleo kwa kufundisha maadili kama vile heshima, umoja, uwajibikaji pamoja na utatuzi wa matatizo kupitia michezo. Tunataka lengo kuu liwe “maendeleo kupitia michezo” na si “maendeleo katika michezo”. Huu ni mtazamo mpya unaolenga kuboresha maadili ya michezo maarufu kama vile soka, netiboli n.k. Lengo kuu si kuwa na ushindani na kujipatia medali. Tunaamini kwamba si rahisi kuielewa falsafa hii tangu mwanzo na ndio maana katika kitabu hiki cha walimu tunatoa ufafanuzi wa dhana hii na michezo ya stadi za maisha inayofundishwa katika warsha.
...
ISBN: 9783000403613
Thank you to Jambo Bukoba
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all